Mar 1, 2011

SHIRIKA LA TAHEA LATOA MISAADA YA MAMILIONI YA SHILINGI KWA YATIMA IRINGA

Mkurugenzi wa shirika la TAHEA na mbunge wa viti maalum(CCM) mkoa wa Iringa Mhe.Lediana Mafuru Mng'ong'o akimkabidhi msaada wa blanket,shuka na godoro mmoja kati ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kijiji cha Tosamaganga kata ya kalenga wilaya ya Iringa leo zaidi ya watoto 100 katika kijiji hicho wamepatiwa msaada huo pamoja na sare za shule na mahitaji mengine toka katika shirika hilo Hapa Mhe.mbunge Mng'ong'o akijaribu kuwauliza maswali ya ufahamu kama wanajua haki zao kama watoto ,hata hivyo watoto hao yatima na wanaoishi katika mazingira magumu waliweza kujibu bila tatizo 'Ndugu zangu wananchi hawa watoto wana akili sana na naomba sana wote tusaidiane kulea watoto hawa' Mkurugenzi wa shirika la TAHEA mkoani Iringa na mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Iringa Mhe.Lediana Mafuru Mng'ong'o (kulia) na diwani wa kata ya Kalenda Emelia Galinoma akishuhudia kazi nzuri ya TAHEA Hapa mbunge akiwa akimshirikisha pia katibu wa CCM kata hiyo na diwani wake kukabidhi msaada kwa mtoto ambaye alidai kuwa utambuzi huo na misaada hiyo ni kazi ya CCM Misaada toka TAHEA Iringa
Walengwa wa Misaada ya TAHEA hawa hapa wakimsikiliza Mhe.Mbunge
Shirika hilo la TAHEA kwa wilaya ya Iringa hadi sasa limefaniki kutoa msaada kama huo katika vijiji vyote msaada wenye thamani ya Tsh.milioni 294 pamoja na kusaidia kiasi cha shilingi milioni 28 kwa ajili ya mfuko wa afya (CHF).
Mkurugenzi huyo wa TAHEA amesema kuwa idadi ya watoto walionufaika na msaada huo ha di sasa ni watoto wote wa vijiji vyote vya wilaya ya Iringa,ambapo watoto 8613 wamenufaika na Afya,Elimu ya msingi watoto 3672,elimu ya Ufundi watoto 64,Elimu ya sekondari watoto 64,malazi watoto 800.
Anasema kuwa hadi sasa magodoro ,mashuka na foronya pea 800 na mablanket 800 yametolewa kwa watoto hao.
Pia maeneo mengine yaliyofikiwa na msaada huo ni pamoja na wilaya ya Mufindi,Kilolo, Njombe ,Ludewa na Makete mchanganua na jinsi ambavyo watoto hao walivyo nufaika utaelezwa katika mtandao huo ambapo utafanya ziara katika wilaya hizo wakati wowote .
Makala maalum ya jitihada za TAHEA Iringa utaipata katika mtandao huu na gazeti endelea kutembelea

(

mkurugenzi wa TAHEA na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa mhe.Lediana Mafuru Mng'ong'o akihimiza wananchi wa kijiji cha Tosamaganga kuendelea kuwasaidia yatima leo

Diwani wa kata ya kalenga Emeria Galinoma akipongeza TAHEA

"