Mar 24, 2011

WIKI YA MAJI MBOZI ILIKUWA HIVI

 Jitwishe mzigo wako uende zako, imani yako imekuokoa!!!! naye akajitwisha ndoo  yake ya maji kisha akatokomea kwao!!! huyu ni mmoja wa akina mama wa Iyula ambaye alishiriki kwenye kunywa maji ya kwanza yaliyovunwa kutoka kwenye tanki lililojengwa katika kituo cha afya cha Iyula kwaajili ya kuvuna maji ya mvua.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ERICK MINGA akionyesha mkono wa kidumu...... baada ya kufungua tanki la maji ya kuvunwa kwa mvua katika kituo cha afya cha Iyula lililogharimu kiasi cha shilingi milion moja unusu, Tanki hilo halitumii teknolojia ngumu na badala yake hutumia raslimali zinazopatikana katika jamii kwa bei ndogo sana kiasi cha kila familia hasa zilizopo wilayani mbozi kuweza kumudu kwakuwa uchumi wa wilaya hiyo unaruhusu kila kaya angalau pato lake kufikia 1.5 milion
 Afisa wa Bonde la Ziwa Rukwa bwana Abdalah Msuya akieleza mpango wa utoaji wa vibali vya matumizi ya maji katika bonde hilo ambapo sasa wanaoendesha miradi ya umwagiliaji, kuchimba visima vya nyumbani na matumizi mengine ya maji wanapaswa kuomba vibali vya matumizi ya maji kutoka bonde hilo, bonde la Rukwa limetoa ofa kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa waombaji kuwa watapewa vibali hivyo bure baada ya kukamilisha taratibu za maombi.
Mhandisi wa maji wilaya ya Mbozi Eng. ACKSON MWASYANGE akizungumzia halmashauri ya wilaya ya Mbozi kushindwa kufikia lengo la asilimia 65% ya wananchi wake kupata maji ifikapo 2010 na badala yake wananchi wanaopata maji safi na salama ni 39% tu. Changamoto kweli kweli