Apr 4, 2011

*BENKI YA BARCLAYS YAFUTA GHARAMA YA HUDUMA KWA WATEJA WAKE WA ATM

Kama picha ya tangazo inavyoonyesha ni kama kupatikana kwa unafuu kwamba sasa mteja wa benki hiyo atashusha pumzi na kupumua baada ya kuondolewa gharama ama ada kwa kutumia huduma ya ATM.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays, Kihara Maina, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa kuwaondolea gharama watumiaji wa huduama za ATM wa benki hiyo, ambapo sasa wateja wa benki hiyo watakuwa wakipata huduma hiyo bure tofauti na awali walipokuwa wakilipia Sh. 600,

uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa benki hiyo, Kati Kerenge (kulia) ni Mkurugenzi wa Huduma za Benki wa benki hiyo, wa Afrika Mashariki na Kati, Zahid Mustafa.
Mkuu wa Mawasiliano wa benki hiyo, Kati Kerenge, akizungumza wakati wa hafla hiyo, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Moven Pick Dar es Salaam leo mchana.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, Rahma na Moni, wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo.
"