Apr 28, 2011

MATOKEO KIDATO CHA SITA YATOKA, WAVULANA SAFARI HII WAONGOZA KUMI BORA


Wavulana wamejitutumua na kufanikiwa kushika nafasi kumi bora katika matokeo ya mtihani wa kidato cha
sita uliofanyika Februari mwaka huu.

Akitangaz amatokeo ya kidato hicho leo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk. Joyce Ndalichako alisema, watahaniwa wamejitahidi kufanya vizuri zaidi katika masomo ya hesabati, kemia, jiografia, fizikia, uchumi na biashara kuliko mitihani iliyopita ambapo wengi walikuwa wakaianguka.

Dk. Ndalichako alisema katika mtihani huo, wavulana 25,872 sawa na asilimia 91.690  na wasichana 15,088
sawa na asilimia 92.63 wamefaulu na kutaja wanafunzi kumi bora walioongoza katika matokeo hayo na majina ya shule zao kwenye mabano kuwa ni Muhagachi Chacha (Kibaha), Samwel Katwale (Mzumbe), Amiri Abdalah (Feza Boys), Aron Gerson, Shaban Omary wote wa Tabora Boys, Kudra Baruti (Feza Boys), George Assenga (Majengo), Comman Nduru (Feza Boys), Francis Josephat (Tabora Boys) na George Felix (Mzumbe).

Dk. Ndalichako pia aliwataja wasichana walioongoza kuwa ni Doreen Kabuche (Benjamin Mkapa), Rahabu
Mwang'amba (Kilakala), Mary Moshi (Kifungilo Girls) Nuru Kipato (Marian Girls) Zainabu Hassan (Al-Muntazir Islamic),Catherine Temu (Ashira), Anthonia Lugomo (Usongwe), Cecilia Mville (Kifungilo Girls), Mariam Matolwa (Kilakala) na Suzan Makoi (Tarakea).

Katika hatua nyingine, Dk. Ndalichako alisema shule za sekondari za seminari zimendelea kufanya vizuri
ambapo kwa mara nyingine shule Marian Girls ya mkoa wa pwani imeendelea kutesa kwa kuibuka ya kwanza katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 30.

Alizitaja shule nyengine zilizo kwenye 10 bora katika kundi hilo kuwa ni Feza Boys, Kifungilo, Kibaha, St.
Mary's Mazinde, Ilboru Tabora St. Mary Goreti, Mzumbe na Mafinga na kwa upande wa shule zilizofanya vizuri katika kundi la zile zilizokuwa na watahiniwa chini ya wanafunzi 30 ni Uru Seminary, St. James Seminary, Maua Seminary, Same seminary Dungunyi Seminary D.C.T Jubilee St. Joseph-Kilocho Seminary, Mlama na Masama Girls.

Dk. Joyce akifafanua kuhusu watahaniwa wa mtihani huo mwaka huu alisema jumla ya watahiniwa 44,720
sawa na asilimia 99.47 kati ya waolisajiliwa walifanya mtihani huo ambapo wasichana walikuwa 16,327 sawa na asilimia 99.63 na wavulana 28,393 sawa na asilimia 99.38, huku kuhusu ubora wa ufaulu akisema jumla ya watahiniwa 34,949 sawa na asilimia 78.53 wamefaulu katika madaraja ya kwanza, pili na tatu wakiwemo wasichana 12,868 sawa na asilimia 79 na wavulana 22,081 sawa na asilimia 78.25.

Alisema watahaniwa 49,653 sawa na asilimia 87.24 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita
mwaka 2011 wamefaulu. Wsichana waliofaulu ni 18,351 sawa na asilimia 88.74 wakati wavulana waliofaulu ni 31,302 sawa na asilimia 86.38. Mwaka jana watahiniwa waliofaulu walikuwa 55,772 sawa asilimia 88.85.

Dk. Ndalichako alisema Baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa watano wa shule na saba wa
kujitegemea waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.

Kwa matokeo hayo Peruzi  www.matokeo.necta.go.tz na www.necta.go.tz au www.moe.go.tz au www.udsm.edu.ac.tz. 
Add starShareShare with noteKeep unreadSend to

    LADY JAY DEE IN STOCKHOLM.

     The Best Female artist in East Africa Lady Jay Dee has Landed in Stockholm Ready for The Biggest Spring Party in Stockholm SPRING BREAK 2011 which will be on Friday night 29 APRIL...

    STOCKHOLM Lets all come together and enjoy the Spring in Style....

    GOOD PEOPLE
    GOOD MUSIC....

    YOUR MOST WELCOME..


    Lady JD akiwa na Promota wake na muandaaji wa onyesho hilo FREDDY ZG SSEBUYOYA aka FREDDYNICE
    Add starShareShare with noteKeep unreadSend to

      NILIKUWA NA HUZUNI LEO SANA....NI KUTOKANA NA KISA CHA HUYU KIJANA...



      Huyu mtoto hapo chini pichani alikuja studio leo toka asubuhi alikuwa hapa,kilichomleta ni kutokana na maisha anayoishi.Mtoto huyu amekuwa akijihusisha na vitendo vya kishoga toka akiwa na miaka 14 akiwa mkoani Tabora na aliyemwanzisha ni bosi katika nyumba aliyokuwa akifanya kazi ya U HOUSE BOY.Yeye ni mwenyeji wa shinyanga ndio kwa wazazi wake mama yake yupo lakini baba hajui alipo alimaliza darasa la saba na kushindwa kuendelea na masomo hivyo akaenda Tobora kutafuta kazi na kupata kazi za ndani.
      Katika nyumba hiyo ilikuwa ni nyumba ya mwarabu ambae amenitajia jina lake ila mie nimelihifadhi baba mwenye nyumba alikuwa akimtaka kimapenzi na kumpa vijiheala lakini hakuwa amewahi kujihusisha nae ila kuna siku mama alisafiri hivyo baba kupata mwanya wa kwenda kumuingilia kinguvu chumbani kwake.Hivyo huo ndio ukawa mwanzo na mchezo mpaka akazowea.

      (sijataka kuweka picha ya uso wake maana kuna waandishi wengine wanaingia humu kuchukua story na kuweka kwenye magazeti,hawachelewi kumbandika huko na kuandika tofauti na nilichokiandika mimi)
      Mama nae akaambiwa na majirani waliokuwa wakihisi jambo na kweli siku ya siku mama akawafumania yeye na huyo baba.Akafukuzwa ndio kuja hapa Dar akafanya kazi za ndani lakini akafukuzwa mwisho akishia katika kuishi kwenye madanguro na mashoga na makahaba na kuamua kuwa anajiuza.Kwa siku zote hizo amekuwa anasutwa na nafsi yake kwamba hicho kitu sio kizuri hivyo akiache mara moja lakini hajaweza kuacha.Kwa hiyo akaamka asubuhi kuja hapa leongo ni kusaidiwa namna ya kuacha.Tumeongea na mwanasaikolojia wetu kasema kama kaamua inawezekana kuacha ila itambidi kubadilisha mfumo wa maisha anayoishi sasa.Kwa upande wa kidaktari bado hatujajua tunalifanyia kazi kama kweli ana nia aweze kubadilika na kuacha.Kiukweli imenisumbua sana kwani ni mdogo ndio kwanza ana miaka 17 sijataka kumhukumu kwani huwezi kujua yajayo kwenye maisha haya mambo hayatabirikiki.Tuna wadogo zetu,ndugu zetu,jamaa zetu kesho watoto wetu nimekaa namtizama alikuwa kafuga na kapaka rangi kucha,amevaa sandals za kike anaongea na kutembea kike.Kwa mujibu wa mwanasaikolojia ni kwamba anatembea na kuongea kike ili kuweza kumpa ishara mwanaume mwingine utofauti wake na mtoto wa kiume wa kawaida.

      Mie najiuliza kuna mtu yoyote unaemfahamu aliwahi kujihusidha na vitendo hivi halafu baadae akaacha...kabisaaaa!!!????inawezekana kuacha huu mchezo?maana huwa inasemekana ukianza ni ngumu kuacha!!!