Apr 30, 2011

MMEA UNAOTUMIKA KUONDOA SUMU ZA MAJI KATIKA NCHI ZA WENZETU -NEMC MPO

Katika safiri safiri zangu ugenini, wakati fulani nilitembelea mji wa mmoja kusini mwa Afrika ambako kuna viwanda vingi, katika eneo la viwanda yanakotiririshwa maji taka nikaona yamepandwa majani haya kwa umbali wa zaidi ya Kilometa tano kuelekea kwenye mabwawa ya maji taka, lakini maji hayo kabla hayajafika kwenye mabwawa yanapitia kwenye mimea hii, nikaelezwa ni mimie hii hunyonya sumu mbalimbali kama chaakula chake kutoka kwenye maji, nikakumbuka Tanzania kando kando mwa mito mingi hasa mkoa wa Iringa kwa uzoefu mimea hii imekuwa ikiota kando kando mwa mito na unakuta mashina yake yanakuwa meusi sana, ni kwasababu ya kunawiri kwa kula sumu inayotokana na miamba ndani ya maji na taka zingine za sumu!!!!!! someni sana kama hamchangii tafiti kama hizi mnapoteza mudaaaaa!