Apr 25, 2011

NMB YATOA POWER TILLER KWA KIKUNDI MBOZI

Ni baada ya ushindi wa muonjo wa kahawa bora kwa mwaka 2011 iliyoshirikisha vikundi zaidi ya 100 nchini kote na Mbozi kuibuka kidedea kwa kuwa na mwonjo wenye ladhaa halisi ya kahawa!!!!


Kiongozi wa kikundi cha Ukusanyaji kahawa cha Mkombozi kilichopo kijiji cha Shiwinga wilayani Mbozi akipokea kombe la Ushindi wa kwanza kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo kwa ubora wa muonjo wa kahawa yake baada ya mashindano yaliyoendeshwa na EAFCA mwezi Februaly mjini Arusha. Mashindano hayo yamekiwezesha kikundi hicho kupata Powertilla ama trekta dogo aina ya Kubota na vifaa vyake, Kombe na Cheti cha Ushindi. Pia mwenyesuti ya blue ni meneja wa NMB Tawi la Mbozi bwana Materu picha na http://www.dtwevetz.blogspot.com/
 
Nje ya NMB Mbozi kulikuwa shwari hivi

Mwali akisubiri kukabidhiwa kwa kikundi cha UKOMBOZI FARMERS GROUP


Fedha zako zinapohitafadhiwa  ni imani pia, hivyo unadhifu wa watumishi ni muhimu katika kuongeza imani kwa wateja, hapa ni watumishi wa benki ya NMB tawi la Mbozi wakiwa wamepozi kwa picha ya pamoja mara baada ya tukio la kukabidhi zawadi hizo.

Pokea Trekta dogo hili iwe kumbukumbu kwa kikundi chenu kwa kuwa wateja wazuri wa NMB mliouza kahawa yenu kupitia utaratibu wa skakabadhi gharani na hatimaye mkashinda katika mashindano ya muonjo wa kahawa 2011" ndivyo anavyoonekana kutamka mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimollo.

 Hotuba mbele ya mwali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! wanakikundi wa MKOMBOZI FARMERS na wadau wengine wa zao la kahawa wakisiliza kwa makini wakati wa makabidhiano ya zawadi ya Trekta dogo iliyotolewa na benki ya NMB kwa kikundi hicho baada ya kuvigalagaza vikundi vingine zaidi ya 100 kutokana na kahawa yake kuwa na muonjo bora 2011
Meneja wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha MBOZI MCCO Bw. Charles Kombe akizungumza na wanakikundi cha Mkombozi katika hafla hiyo. PICHA ZOTE NA http://www.dtwevetz.blogspot.com/