May 20, 2011

TAARIFA ZAIDI ZA MAUAJI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI RUNGWE

Jumla ya watuhumiwa 4 wanashikiriwa na polisi wilayani Rungwe wakihusishwa na mauaji yaliyotokea jana usiku.
Mauaji hayo yalifanywa nyumbani kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe John Mwankenja ambaye alipigwa risasi tatu kwenye paji lake la uso na kusababisha kifo cha kutisha baada ya kufumuliwa kwa kichwa chote na kusambaza ubongo kwenye gari lote.
Akizungumza na  wanahabari wilayani Rungwe mkuu wa wilaya ya Rungwe Jackson Msome amesema bado wanaendelea kuwasaka watu wengine wanaohusishwa na tukio hilo na kwamba serikali kupitia vyombo vya usalama inawaomba wananchi kutoa ushirikiano utakaowezesha kukamatwa kwa watu hao.

Amesema watuhumiwa wanne wanaisaidia polisi wakati uchunguzi ukiendelea.

Naye Mbunge wa viti maalumu Mkoani Mbeya Hilda Ngoye ambaye ni jirani  wa marehemu amesema tukio hilo linaashiria kutoweka kwa ustaarabu wa majadiliano katika jamii kwani mauaji hayo yanadhihirisha wazi kuwa yalikuwa ya kudhamiriwa na si majambazi.
Nao vijana wanaoishi na marehemu Mwankenja wameeleza kuwa tukio hilo lilihusisha wauaji watatu ambao walikuwa wamejificha katika maeneo ya mbele ya nyumba na wengine wakiwa kwenye migomba ambapo waliwaamuru watoto waliokuwa wanashusha mizigo kwenye gari hilo akiwa tayari ameshashuka.
Habari zaidi zinahusisha masuala ya kisiasa ambapo inadaiwa kati ya waliokamatwa mmoja wao ni miongoni mwa walioshindania kiti cha udiwani katika uchaguzi uliopita.
imeelezwa zaidi kuwa mwezi uliopita Mwankenja alikuwa ameshinda kesi ya uchaguzi ilifunguliwa dhidi yake na wagombea wa vyama vya TLP na CHADEMA katika kinyang'anyiro cha Udiwani ambapo mahakama ilitoa hukumu kuwa Mwankenja alikuwa ameshinda kesi hiyo.
BAADHI YA MASHUHUDA WA TUKIO HILO PAMOJA NA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE  JACKSON MSOME , MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA MBEYA HILDA NGOYE WAKIZUNGUMZIA MAUAJI HAYO
VIDEO YA PILI INAONYESHA WAOMBOLEZAJI NA MAREHEMU JOHN MWANKENJA WAKATI AKIZUNGUMZA JUZI KWENYE KIKAO CHA BARAZA  LA MADIWANI AKIWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA
kwa taarifa zaidi fualtilia video hizi