May 23, 2011

UZINDUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MWANASHERIA MKUU

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema (kushoto) akiongea na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mkutano  wa baraza la wafanyakazi wa ofisi yake mara baada ya kumalizika kufunguliwa kwa mkutano huo. Mkutano huo wa siku mbili ulifunguliwa leo na waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani  katika Hoteli ya Giraffe Ocean View jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Sheria Hamis Msigala akimkabidhi risala ya wafanyakazi Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani huku Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju akishuhudia. Waziri Kombani alifunga leo mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi la ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali unaofanyika   katika Hoteli ya Giraffe Ocean View jijini Dar es Salaam

Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani akimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema mara baada ya waziri huyo kumalizia kufungua mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi la ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali unaofanyika   katika Hoteli ya Giraffe Ocean View jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kufunguliwa kwa mkutano wao mkuu. Watatu kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani akifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema na watano kutoka kulia ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali wakifuatilia kwa ukaribu hotuba ya ufunguzi wa mkutano wao iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani (hayupo pichani). Mkutano huo wa siku mbili unafanyika   katika Hoteli ya Giraffe Ocean View jijini Dar es Salaam. Picha na Anna Nkinda - Maelezo