Jun 25, 2011

BARAZA LA MADIWANI MBOZI LATISHIA KUKAMATA WATAKAOJIPENDEKEZA KUNUNUA KAHAWA MBICHI WILAYANI HUMO

Waheshimiwa madiwani wa baraza la Mbozi wakifuatilia mjadala katika kikao cha kufunga mwaka wa fedha wa serikali ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kusitisha mara moja ununuzi wa kahawa cheri baada ya kubainika kuchangia kushusha ubora wa zao hilo na kuwapunja wakulima

Kamati ya uchaguzi ikihesabu kura za nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambapo madiwani wawili walikuwa wakiwania nafasi hiyo kutoka vyama vya CHADEMA  na CCM

Mgombea wa nafasi ya Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Mbozi MH Mwesya kutoka Kata ya Tunduma akiwa amepozi kusubiria matokeo ya kura za uchaguzi huo ambapo aliweza kuambulia kura 7 kati ya 43 zilizopigwa

Mh Bernard Sichilonga Diwani wa Ivuna akisubiria Matokeo ya uchaguzi wa nafasi aliyokuwa akiitetea ya Makamu mwenyekiti  ambapo aliibuka na ushindi wa kura 36

Katibu TawalaWilaya ya Mbozi Leonard Magacha akisisitiza mpango wa kukamata watu watakaojihusisha na ununuzi wa kahawa mbichi

Mwenyekkiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Elick Minga aklitangaza rasmi vita dhidi ya makampuni yanayonunua kahawa Mbichi wilayani humo ambapo imeelekezwa kuwa wananchi wachukue uamuzi ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola na mwanasheria wa  halmashauri hiyo atasimamia mashauri hayo