Jun 16, 2011

KUPATWA KWA MWEZI KWAJITOKEZA UINGEREZA

Wakazi wa nchini Uingereza usiku wa kuamkia leo walipata fursa ya kuona kupatwa kwa mwezi ambapo mwezi huo ulionekana"mwekundu kama damu" kwa takriban dakika 100. Hata hivyo, wanasayansi wa taasisi ya mambo ya anga ya Marekani (NASA) walieleza kuwa wakazi wa Ulaya hakufaidi vizuri tukio hilo kwani ulionekana kabla ya mwezi kuchomoza kulingana na ya huko nchi za Ulaya)

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kupitia mtandao wa barua pepe tukio hilo lilianza saa 12 na dakika 24 jioni kwa muda wa majira ya joto ya nchini Uingereza (1824 British Summer Time) na kuendelea hadi saa 6 usiku (0000 BST) lakini kwa Uingereza ulianza kuonekana saa 3 na dakika 19 usiku (2119 BST).

Aidha wakazi wa maeneo ya nusu ya mashariki ya bara la Afrika, eneo la Mashariki ya Kati, Asia ya Kati na magharibi mwa Australia pia waliweza kuliona tukio zima kwa takribani dakika 100 za kupatwa kwa mwezi. Hata hivyo, wakazi wa Marekani hawatoliona tukio hilo kwa vile litatokea majira ya mchana kwa nyakati hizo.

Kijiografia, asili ya mwanga wa mwezi ni mionzi ya jua. Tukio la kupatwa kwa mwezi ni pale Dunia, Jua na Mwezi zinapokuwa mstari mmoja, na kivuli cha Dunia kinaangukia kwenye Mwezi kamili. Uwekundu kama damu katika tukio hilo la leo ni matokeo ya miale ya jua kupita Duniani kisha kuangukia kwenye uso wa mwezi…(Rashid Mkwinda kwa Msaada wa vyanzo mbalimbali vya habari