Jun 5, 2011

NIMEPENDA MAISHA YA MZEE MCHUNGAJI MSTAAFU MWAISANGO

Mchungaji Mwaisango akelezea mambo aliyoshuhudia akiwa kijana wakati ule wa kupata uhuru, anasema Wakristu kwa miaka hiyo walikuwa wamepiga hatua kubwa sana kutokana na kuwa na shule nyingi lakini baadaye Nyerere kwa kutambua tofauti ya elimu katika makundi ya jamii aliamua kuzitaifisha shule nyingi za kikristo na kuwa za serikali ambazo zikawa zikitumika kwa watanzania wote.

Miaka 50 ya Uhuru: Anaeleza kuwa Uzalendo umepungua sana na hii inatokana na kuwepo kwa pengo kubwa kati ya wenye nacho na wasio nacho, hali hii anaeleza kuwa ni hatari kwakuwa inaweza kumwingiza mtu kwenye matukio mabaya kwakuwa anajua hakuna anachopoteza! anashauri watumishi wa serikali warejee kwenye misingi, enzi zile mtumishi anajisikia faraja akimtatulia mwananchi shida yake lakini sasa mtumishi anajisikia kero kutatua shida ya mwananchi!!!
Mchungaji huyu ameamua kupumzika kazi ya bwana na sasa anafanya kazi kwa kujitolea na consultancies akiwa ametulia kijijini kwake Katumba II ambapo imekuwa kama eneo la matibabu kwa wagonjwa kutokana na watu kufurika kwake kwenda kuomba ushauri mbalimbali kutokana na changamoto za kimaisha na masuala mazima ya maendeleo. Anakumbukwa kwa uongozi wake kwenye kanisa la Moravian jimbo  la Kusini akiwa Katibu Mkuu