Jun 10, 2011

Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mbeya katika mdahalo kesho ukumbi wa Royal Zambezi.

WAGOMBEA 11 wanaowania nafasi ya Uenyekiti wa Chadema mkoa wa Mbeya kesho wanatarajiwa kuhudhuria mdahalo ulioandaliwa na Umoja wa wanafunzi wa Chadema (CHASO) tawi la Teofilo Kisanji.
Akizungumza na mtandao huu katibu mkuu wa umoja huo Chadema Student Organization (Chaso) katibu wake Atupele Elias amesema mdahalo huo una baraka zote kutoka kwa Katibi mkuu wa Chadema Taifa Dr, Wilbroad Slaa.
Atupele amesema baraka hizo walizipata kwa njia ya simu na walitakiwa kumwandikia barua kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi ambapo wameandika barua hiyo na kusainiwa na viongozi wa umoja huo.
Katibu huyo wa Chaso amesema lengo la mdahalo huo ni kuimarisha demokrasia na kwamba wajumbe na wananchi wanatakiwa kuwapima uimara wa wagombea kabla ya uchaguzi kwa nia ya kufanya maamuzi sahihi na kwamba pia mdahalo huo utawasaidia wagombea ambao hawana uwezo wa kusafiri kwa ajili ya kwenda wilayani kushawishi wajumbe.
Mbali na katibu huyo wa Chaso, akizungumza na mtandao huu wa www.kalulunga.blogspot.com Katibu wa Chadema mkoa wa Mbeya Eddo Mwamalala amesema kuwa siku ya mwisho ya kurejesha fomu za kiti hicho ilikuwa Juni 4 mwaka huu ambapo wanachama 11 wamerejesha fomu hizo. Aidha alisema kuwa chama hicho kimefurahishwa na kujitokeza kwa wanachama hao ambapo awali chama hichio kilikuwa kinawaomba na kuwabembeleza wanachama kuwania nafasi kama hiyo lakini kwa sasa wengi wao wanajitokeza wenyewe. Aliwataja waliochukua fomu kuwa ni pamoja na Herode Jivava, Geprge Mtasha, Philip Mwakilima, Sorwa Ngea, John Mwambigija, Hugho Kimario, Lucas Mwasikili, Joseph Mwachembe, Aminika Mwihomeke, Zabron Nzunda na John Ngeka. Sanjari na hayo alisema kuwa Viongozi wote kutoka wilaya zote Nane na majimbo ya uchaguzi ndiyo watakaohusika kumchagua kiongozi huyo itakapofika Juni 20 mwaka huu. CHANZO> KALULUNGA.BLOGSPOT.COM Mwisho.
"