Jul 15, 2011

HAKIMU WILAYA YA MBOZI ANASWA NA VIPODOZI HARAMU


HAKIMU mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mbozi Bi. Nyasige Kanjanja(38) amekamatwa kwa mara nyingine akiwa na vipodozi ambazo ni bidhaa zinazodaiwa kuwa zimepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu.

Hakimu huyo ambaye mwanzoni mwa mwezi April alidaiwa pia kukutwa na vipodozi haramu na kesi yake bado iko katika mahakama ya wilaya ya Mbeya anadaiwa kukamatwa Julai 14 majira ya saa 9.00 alasiri maeneo ya Iwambi katika jiji la Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Bw. Advocate nyombi alisema kuwa Hakimu Kajanja alikamatwa akiwa anaendesha gari aina ya Honda yenye namba za usajili T 999 BDK.

Bw. Nyombi alisema kuwa maofisa wa Mamlaka wa Mapato mkoa wa Mbeya ambao walikuwa katika doria walimkamata mtuhumiwa akiwa na mtu mwingine aliyekuwa abiria katika gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Zena Mwakamela(30).

Alisema ndani ya gari yake kulikutwa vipodozi aina mbalimbali ambavyo vimepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu pamoja na sabuni aina ya Boom boksi moja ambayo inadaiwa kuingizwa nchini bila kibali cha Mamlaka ya Mapato.

Kamanda Nyombi alisema kuwa hata hivyo mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani jana mchana.

Mwanzoni mwa mwezi April Maofisa wa Mamlaka ya Mapato mkoani Mbeya walimkamata Hakimu huyo maeneo ya Iyunga Jijini Mbeya akiwa na vipodozi vinavyodaiwa kuwa ni haramu ambapo alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya na kesi yake bado inaendelea.
Ilidaiwa mahakamani hapo  kuwa mshtakiwa alitenda kosa hiko Aprili
mosi mwaka huu katika maeneo ya Iyunga akiwa na gari yenye namba za
usajiri T.171 AUG aina ya SUZUKI ESCUDO ambayo ilikuwa ikiendeshwa na
mshtakiwa.

Aidha kwa mara ya kwanza mshtakiwa alifikishwa mahakamani hapo Aprili
28 mwaka huu na mshtakiwa alikana kosa na jana alifikishwa tena ili
kujibu mashtaka hayo lakini bado aliendelea kukana mashtaka  hayo.

Tangoh aliweza kutoa maelezo ya awali ya mshtakiwa jinsi alivyokamatwa
na mamlaka ya mapato TRA alianza kwa kueleza kuwa mamlaka hiya ilipata
taarifa kutoka kwa watu wa mipakani na kuelekezwa kuwa gari yenye
namba tajwa hapo juu ilikuwa ikitiliwa shaka na ndipo mamla hiyo
ikaanza kuifatilia.

Maofisa wa mamlaka wa mapato TRA waliifatilia wakaweka ulinzi maeneo
ya Mbalizi na walipoisimamisha gari huyo maeneo hayo gari hiyo
haikusimama badala yake mshtakiwa aliongeza mwendo na ndipo mamlaka
hiyo iliamua kumfuatili nyendo zake mshtakiwa huyo kwa nyuma.

Mshtakiwa alipofika maeneo ya Iyunga aliamua kuingia mitaani huko
aliendesha gari hiyo kwa  kasi na kugonga pikipiki na sturi ya muuza
nyanya  na baadaye aligonga nyumba ya mrs Ndondwa na hapo aliamua
kuacha gari na kukimbia.

Baada ya muda mfupi alirudi na akachukuliwa yeye pamoja na gari yake
maofisa hao wa TRA  mpaka Malawi Cago tawi la mbeya na kukagua gari
hiyo mbele ya mshtakiwa

Tangoh alisema kuwa walipokagua ndani ya gari hiyo walikuta vipodozi
vikiwa vimefichwa sehemu mbalimbali katika gari kwenye gunia la
mkaa,kwenye mifuko ya baadhi ya viti na chini ya viti vya gari.

Baadhi ya vipodozi vilivyokutwa ni
carorit,Carotte,Top-lemon,Pro-light,Princes
clair,Dipron,Betasol,Epider lotion,Diroson na pure grycerin vyote
vikiwa na dhamani ya shilingi 2milion.

Baada ya kufanyiwa upekuzi mamlaka hiyo ilichukuwa baadhi ya  vipodozi
na kupeleka mamlaka ya chakula na dawa(TFDA) ili vifanyiwe uchunguzi
na majibu yalibaini kuwa bidhaa hizo zina kemikali zinazokatazwa.

Mshtakiwa alikanusha maelezo hayo na hakimu alihilisha kesi hadi may25
mwaka huu.

RASHID MKWINDA-MBEYA