Jul 22, 2011

ELIAKIM CHACHA MASWI ACHUKUA NAFASI YA JAIRO, WADAU WA TAMISEMI WAMLILIA

BW. ELIAKIM CHACHA MASWI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kufuatia Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Bwana David K. Jairo, kupewa likizo kwa muda, Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L. Luhanjo, amemteua Bwana ELIAKIM CHACHA MASWI, kuwa KAIMU KATIBU MKUU, Wizara ya Nishati na Madini kuanzia leo tarehe 22 Julai, 2011. Bwana MASWI, kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.Imetolewa na Premi Kibanga,Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,Ikulu.Dar es salaam.22 Julai, 2011
Katika mazungumzo ya hapa na pale kuzungumzia mabadiliko hayo wadau wengi wa TAMISEMI wameonekana kumlilia bwana Maswi kutokana na misimamo yake na utendaji wake ambao uliwezesha halmashauri za wilaya kuchakarika hapa na pale kuhakikisha kuwa zinajiimarika kwa kutenda vyema katika huduma zake kwa wananchi.
wanaeleza kuwa jamaa alikuwa mkali pale anapobaini uzembe na pia hakuwa na lugha za kuficha ficha kwenye makosa na alikuwa akiwafikishia ujumbe moja kwa moja wahusika pasipo kusikiliza majungu hatua ambayo wapiga majungu walikuwa wakiongopa kupiga hodi TAMISEMI kwenda kuchonga umbeya usio na uthibitisho. Kila lakheri Maswi katika ofisi mpya tunakuombea kila lililozuri! Mungu atakuangazia majukumu yao na uongozi wako utukuke!
"