Jul 8, 2011

Kansela Merkel aitetea serikali kubakia kimya

"Syria
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametetea msimamo wa serikali yake kubakia kimya kuhusu biashara ya vifaru inayodaiwa kufanyika na Saudi Arabia na iliyozusha mabishano makali nchini humu.
Kansela Merkel ameliambia gazeti la Kijerumani, 'Mittelbayerischen Zeitung' kuwa kuna sababu nzuri za kuweka siri maamuzi yanayopitishwa katika baraza la kitaifa la usalama. Lakini uwazi unaotakiwa, unapatikana katika ripoti ya biashara ya silaha inayotolewa kila mwaka. Inadaiwa kuwa Saudi Arabia inauziwa vifaru 200 vya chapa ya 'Leopard 2'.
Vyama vya upinzani vya SPD, Die GrĂ¼ne na Die Linke vinapinga biashara hiyo vikielezea ukiukaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia. Mada hiyo itajadiliwa tena hii leo katika bunge la Berlin. Chama cha Die Linke kimetoa mwito kwa serikali kuzuia biashara hiyo ya
"