Jul 21, 2011

MATUKIO KUTOKA SONGEA




Mchuuzi wa bidhaa za mikononi maarufu machinga,akitembeza kofia mitaani kwa ajili ya kutafuta wateja kama alivyokutwa katika mtaa wa matomomndo manispaa ya songea jana,


Kijana anayejishughulisha na kuuza bisi katika mitaa mbalimbaliAbbas Yassin akiwa na dishi lenye bisi hizo baada ya kuondolewa stand kuu ya mabasi mjini songea kufuatia halmashauri ya  manispaa  ya songea kutaka kuifanyika ukarabati mkubwa stand hiyo,ambapo baadhi yo ulamika kuzunguka katika mitaa mbalimbali mjini hapa,

Askari mgambo wa manispaa ya Songea, Sponsa Haule kulia,na Kardo Luambano kushoto, wakiwa na vyombo vya mama lishe mmoja hayupo pichani baada ya kumkamata akifanya biashara ya kuuza chakula kwenye maeneno yasiyoruhusiwa mjini songea jana,katikati ni Bw afya wa maniya Songea Kassim Mchata

Mpiga picha wa kujitegema BW Ahmad Mvulla,akiuchapa usingizi baada ya kusubiri wateja kwa muda mrefu bila ya mafanikio katika studio ya ABBAS Mjini songea jana,biashara ya upigaji picha imekuwa ikipungua siku hadi siku kufuatia kuwepo kwa kamera nyingi katika baadhi ya familia hapa

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Majengo katika Manispaa ya Songea wakila askrim kwa ajili ya kupoza kiu kufuatia kukosekana kwa bomba la maji safi na salama shuleni hapo jana,

Muosha viatu maarufu mjini Songea anayefahamika kwa jina moja la Chikulubu,akiosha moja ya viatu vya wateja wake,uoshaji wa viatu wa aina hii usiozingatia kanuni za afya ni  unaweza kusababisha maambukizo ya magonjwa mbalimbali,
PICHA ZOTE NA AMRI MUHIDIN