Jul 17, 2011

MGOMO WA MADEREVA WA MAROLI WACHEMSHA NCHI



Mgomo ulioanza leo hii ukihusisha madereva wa maroli yanayobeba bidhaa na mafuta kwenda nje ya nchi kutoka bandari za hapa nchini unaiweka nchi mahala pasipo salama.
Taarifa zilizopatikana kutoka mipaka ya Horiri, Tunduma, Kasumulu na baadhi ya vituo vya TRA ikiwemo Kahama zinaonyesha kuwa usajiri na upitishaji wa nyaraka ambao hufanywa kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana kwa siku ya leo haukuhusisha kabisa magari yayatoka kwenda nje bali yanayoingia.
Magari yaliyosainiwa nyaraka zake wakati wa kutoka nje ya nchi ni yale tu yanayoendeshwa na madereva kutoka nje ya nchi.
Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa madereva hao Mohamed Fikiri amesema anaamini ujumbe wao utasikika kupitia utaratibu huo na kwamba wasingependa kuyumbisha uchumi wa nchi bali ni kutokana na maisha yao kutothaminiwa na wenye mali.
Naye makamu mwenyekiti wa Madreva hao Bwana Richard Nyagawa ambaye yupo Tunduma kwa sasa kuratibu mgomo huo amesema hadi kufikia mchana huu mgomo wao umekuwa wa mafanikio kutokana na kutokuwepo kwa gari lililokuwa likivuka kwenda Zambia linaloendeshwa na watanzania.
Napenda kukuthibitishia bwana Mwandishi kuwa yale tunayoyataka yatazingatiwa najua serikali imekaa kimya kwa siku moja wakijua mgomo huu ni wa leo tuu lakini taarifa ni kwamba hii ngoma inaendelea mpaka tusikilizwe, alisema bwana Nyagawa