Jul 20, 2011

MKUTANO WA MKUU WA MKOA NA MADEREVA TUNDUMA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya John Mwakipesile akizungumza na Madereva wa magari yanayobeba mizigo kupeleka nje ya nchi , ambapo amesema malalamiko yao yatashughulikiwa kwa utatu unaohusisha wamiliki kupitia chama chao, umoja wa madereva na serikali kupitia wizara ya Kazi . Wakati mwingine alilazimika kupanda jazba kutokana na madereva hao kukataa kukubaliana naye kuendelea na safari ama kurejesha magari kwa matajiri wao!

Kamati ya Uongozi wa madereva hao wakiwa wanasikiliza maeelezo kutoka kwa uongozi wa mkoa ambao ulifika kuwakilisha baadhi ya yale yaliyozungumzwa kati ya mkuu wa mkoa na waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda

Katibu wa madereva kushoto akiwa na Mkuu wa mkoa na kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo

Makamu mwenyekiti wa umoja wa Maderva hao Bwana Richard Nyagawa akizungumza na Blog hii

Meneja wa TRA Mkoa(Forodha) Bwana Logacian Shirima akizungumzia baadhi ya mabadiliko yaliyofanywa na TRA kutokana na madai ya madereva hao yaliyofikishwa kwa kamishna mkuu  wa TRA. Indaba blog ilikuwa huko ikifuatilia Miongoni mwa maamuzi yaliyofikiwa ni pamoja na kuongeza siku za kusafiri kutoka Dar e salaam hadi Tunduma ambako sasa itachukua siku 7 badala ya Tano za awali na kwamba lengo ni kuwaepusha na matukio ya uhalifu kwa baadhi ya maeneo ambako  kuna matukio ya uhalifu mfano milima ya Ihemi mkoani Iringa , Nyororo  na  Maeneo mengine  na kwamba wamekuwa wakiendesha magari usiku kutokana na kuhofia kupigwa faini na mamlaka ya mapato kutokana na muda wanaopangiwa kutotoshereza! Huyu walimpigia makofi ya kushangilia kutokana na tamko hilo

OCD MBOZI Afande Ernest Dudu akizungumzia utaratibu wa Trafic kusimamisha maroli ambapo alitangaza rasmi kuwa kwenye wilaya yake magari yanayokwenda nje ya nchi yatafanyiwa ukaguzi kwenye mizani tu ambapo kuna mizani moja katika wilaya hiyo eneo la Mpemba,

Kimbembe kilianzia hapa baada ya viongozi kupanda jukwaaani kwa lengo la kuwashawishi madereva waanze kurejea kazini  wakati wao wakifuatilia masuala yaliyobakia kwa  waziri mkuu, ambapo ghafla hali ya hewa ikachafuka ambapo wakataka kuwashusha viongozi wao kwa kushindwa kutamka la maaana! hali imeendelea hivyo hivyo leo ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ADVOCATE NYOMBI amepiga kambi huko.