Jul 1, 2011

SONGEA JIONI YA LEO NA MWANDISHI WETU MUHIDIN AMRI (NDOLANGA)

Chinga hawa wakikatiza mitaa mjini Songea kutafuta riziki!!

Ghuba likiwa limejaa uchafu ambao haujazolewa kwa muda mrefu jirani na Ofisi ya mganga Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,haikuweza kufahamika mara moja sababu ya msingi iliyofanya uchafu huo kuwa hapo kwa muda mrefu,

Mfanyabiashara wa viatu vya Mitumba katika mtaa wa Sokoni mjini Songea  Bakari Ali,akipanga  viatu hivyo kwa ajili ya kuwavutia wateja  wanaopita katika huo mtaa huo,kumekuwepo na ongezeko kubwa  la watu wanaotumia bidhaa za mitumba kuliko vile vya madukani hasa kufuatia kuingizwa kwa wingi bidhaa za kichina ambazo baadhi ya hizo zimekuwa hazina ubora wa kutosha, burudani ni pale yeye mwenyewe amejipigia Yebo Yebo halafu anauza buti kali!!!!

Soko la la wakulima wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma lililopo  kando kando ya barabara kuu ya Natumbo Tunduru likiwa limeachawa bila kufanyiwa ukurabati  licha ya halmashauri hiyo kukusanya ushuru kutoka kwa wafanyabiashara wake


Magunia ya mchele yakiwa yamefunikwa kufuatia wafanyabiashara wake kugoma kutoa huduma hiyo wakigomea ongezeko la kiwango cha ushuru wanaotakiwa kutoa kwa halmshgauri ya manispaa ya songea,ambapo umeongezeka kutoka tshs 200 hadi 400,


Meza za wafanyabiashara zikiwa tupu bila bidhaa yeyote kufuatia wafanyabiashara hao kugoma baada ya kuongezewa ushuru na manispaa ya songea kutoka tshs 200 hadi 400,

Ghuba likiwa limejaa uchafu ambao haujazolewa kwa muda mrefu jirani na Ofisi ya mganga Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,haikuweza kufahamika mara moja sababu ya msingi iliyofanya uchafu huo kuwa hapo kwa muda mrefu,