Jul 20, 2011

TAARIFA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE, HALI YA TUNDUMA NI TETE

Taarifa zilizotufikia dakika chache zinaonyesha kuwa hali ya hewa Tunduma inaelekea kuchafuka wakati wowote kutokana na madereva wa magari makubwa kulazimishwa kuondoa magari yao na kuendelea na safari.
Taarifa zilizotolewa na viongozi wa Madereva hao zinasema kumekuwa na hali tete kutokana na makubaliano ya jana kuonekana kutokubalika kwa miongoni mwa madereva kuwa magari yaliyokuwa yakienda nje ya nchi  yaendelee na safari.
Madereva hao wanataka mgomo kuendelea na hivyo kuanza kuwashambulia viongozi wao  wakidai wamewasaliti kwa kukubaliana na mkuu wa mkoa jana ambaye alifika kwa lengo la kuzungumza nao na kuwataka kuendelea na safari zao wakati suala hilo likishughulikiwa.
Tayari kuna taarifa kuwa gari moja la mizigo lililokuwa likivuka kwenda Zambia limepigwa mawe na kuharibiwa kioo dakika chache zilizopita, hatua ambayo viongozi wa madereva hao wamelazimika kwenda kujisalimisha polisi ili kuomba msaada zaidi kuweza kusimamia magari yanayovuka yavuke salama.
Wakati hayo yakitokea tayari kikosi cha FFU kimepiga kambi Tunduma kufuatilia suala hilo kwa lengo la kutuliza chochote kitakachojitokeza
Indabaafrica itaendelea kuwajuza kinachojiri kila dakika