Jul 17, 2011

wanahabari watembelea bwawa la kuzalisha umeme la mtera na kujionea hali ilivyo mbaya

wanahabari watembelea bwawa la kuzalisha umeme la mtera na kujionea hali ilivyo mbaya: "
waandishi wa habari wakiwa katika ziara ya Mtera wakipata mawelezo ya awali
ni Mhandisi Mkuu wa Uendeshaji kutoka kituo cha kuzalisha umeme kwenye bwawa la Mtera, Julius Chomolla akitoa maelezo kuhusu kipimo cha kuonyesha maji yamejaa katika eneo hilo. Katika kiuto hicho kiwango cha juu cha kuzalisha umeme ni mita 698 wakati cha chini cha kuzalisha nishati hiyo ni mita 690 na jana (juzi) kipimo hicho kilionyesha mita 690.74, ambapo. Bwawa hilo linazalisha umeme MW 33 badala ya MW 80.
Mhandisi Mkuu wa Uendeshaji kutoka kituo cha kuzalisha umeme kwenye bwawa la Mtera ,Julius Chomolla akionyesha kipimo cha kuonyesha maji yaliyopungua.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiangalia jinsi bwawa la Mtera ilivyopungua maji
Wanahabari wakitembelea bwawa la Mtera
waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari wakipata maelezo ya uzalishaji wa umeme katika kituo cha Mtera.
BWAWA LA MTERA HALITOSIMAMISHWA KUZALISHA UMEME JAPO KINA CHA MAJI KIPO CHINI KABISA
Picha na Habari na
Magreth Kinabo - MAELEZO
IMEELEZWA kuwa bwawa la Mtera halitosimamishwa kuzalisha umeme kutokana na kupungua kwa kina cha maji kilichosababishwa na ukosefu wa mvu za kutosha. kauli hiyo ilitolewa jana na Mhandisi Mkuu wa Uendeshaji wa kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera ,Julius Chomolla wakati akizungumza na waandishi wa habari jana(juzi). ' Utaratibu unafanyika wa kuzalisha umeme kwa masaa katika bwawa hili ili uzalishaji usisimame kama ilivyotokea mwaka 2006. hivyo tutaendelea kuzalisha umeme bila ya kusimama hadi tutakapofiklia msimu ujao wa mvua,' alisema Chomolla. Chomolla aloiongeza kuwa kiwango cha umemekinachozalishwa kwa sasa hadi jana(juzi) katika bwawa hilo ni MW 33 badala ya MW80 . Aliongeza kuwa kiwango cha juu toka usawa wa bahari cha kuzalisha umeme ni mita 698.50 na cha chini mita 690, ambapo siku ya jana(juzi) kilikuwa mita 690.74. kituo hicho KINAtegemea maji kuto mito miwili ambayo ni Ruaha Mkubwa na Ruaha na Mdogo na Kisigo wakati wa kipindi cha masika. Kwa mujibu wa Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) ,Badra Masoud Vituo vbingine vinvyozalisha umeme ni Kihansi kwa sasa ni MW 90 badala ya MW 180,Kidatu MW 40 badala ya 204, New Pangani MW 20 badala ya MW168 na Nyumba ya Mungu ni MW3.5 badala ya MW 8.
"