Aug 7, 2011

MAELFU WAJITOKEZA KUMZIKA MZEE WETU DUNSTAN MGANI MTITU

Picha ya Mzee wetu Marehemu Dunstan Lugagile Mtitu Mgani ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 61

Mwili wa marehemu ukiwa mbele ya familia na waombolezaji wengine kwenye kanisa la ANGLICAN la  Mtakatifu Andrew mjini Njombe

Familia ya Marehemu Dunstan Mgani ikiwa imelizunguka jeneza kabla ya kuelekea makaburini eneo la Mji mwema kwaajili ya kuhifadhi mwili wa marehemu kwa pumziko la milele mpaka ufufuo wake.

Makasisi wa Kanisa Anglican Njombe wakiwa wamelizunguka kaburi kwaajili ya maombi

Padre Almas ambaye aliongoza ibada ya mazishi akisisitiza jambo kwa watu waliofika kumsindikiza mzee wetu kwenye pumziko la milele

Familia ya Mzee Mgani ikiongozwa na Mtoto wake wa kwanza bwana Oscar Mgani wa kwanza kulia pamoja na waumini wenginewaliomiminika kwenye kanisa la Mtakatifu ANDREA mjini Njombe kushiriki ibada ya kumuaga mzee huyu ambaye anaelezwa kuwa alikuwa kiungo muhimu baina ya kanisa, waumini na jamii kwa ujumla katika mji wa Njombe na vitongoji vyake.

Ni sehemu tu ya watu waliofika makaburini kushiriki mazishi ya MZEE MTITU DUNSTAN MGANI ambapo kwa hesabu ya haraka magari yaliyoshiriki kwenye msafara ni zaidi ya 300 hatua ambayo baadhi ya watu waliotarajiwa kushiriki kwenye mazishi walishindwa kufika kwa wakati na kuwasili makaburini wakati wengine wakitawanyika kutokana na msongamano wa magari kwenye barabara ya Njombe -Songea ambako msafara huo ulipitishwa kuelekea makaburi ya mji mwema.

Askofu wa Kanisa Anglican Njombe pamoja na Canon Mwafute wakiweka shada la maua kwa pamoja kwenye kaburi la mzee Dunstan Mgani juzi mjini Njombe