Sep 7, 2011

BARAZA LA MADIWANI MBOZI HALI YA HEWA YACHAFUKA, DC ASHAMBULIWA KWA MATUSI

Baadhi ya madiwani wakiwa katika kikao cha leo, ambacho kimemalizika kwa kulazimishwa kupiga kura za kutaka mabadiliko ya mapendekezo ya makao makuu ya wilaya ya Momba, ambapo kulijitokeza hali ya kushambuliana kwa maneno na matusi!
Timu ya watalaamu waliofanya upembuzi wa mapendekezo ya makao makuu ya wilaya na tathmini ya uendelezaji wa mipango miji katika maeneo ya matano ya wilaya ya Momba ambao wameshambuliwa kwenye kikao hicho kuwa walitaka kuibeba Ikana -Ndalambo kuwa ndilo eneo stahiki!.

Mkuu wa wilaya akisindikizwa kwa Ulinzi baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Madiwani huku wandishi wakiwa wamemganda wakitaka waelezwe kilichompelekea kusoma barua ya siri kutoka Chama cha mapinduzi iliyomtaka ashawishi kufanyika mabadiliko ya makao makuu ya wilaya kutoka Ikana na kuwa Chitete, Barua hiyo ilikanwa na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya Bwana Mkondya kuwa haijawahi kujadiliwa na kikao cha kamati ya siasa ya CCM Wilayani humo.

Macho ya diwani huyu yanaonyesha hali ya mashaka kwenye kikao hicho kilichoishia kwa baadhi ya madiwani kuporomosha matusi huku Dc akiuchuna kama vile siye yeye anayetukanwa.

Mkuu wa wilaya ya Mbozi GABRIEL KIMOLO akifungua mkutano wa baraza maalumu la madiwani ambapo katika kufanya ushawishi akajikuta anasoma barua ya siri iliyoandikwa kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ikimwelekeza kushinikiza kuitishwa kikao cha dharura cha madiwani na kufikia maamuzi ya kuteua Chitete kuwa makao makuu ya wilaya, barua ambayo baadaye ikageuka kuwa shubiri kwenye kikao hicho baada ya DC kutakiwa afafanue barua na maoni ya wdau wengine yako wapi na nini kimemsukuma asome ya CCM peke yake?

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi ERICK MINGA AMBAKISYE alikumbana na wakati mgumu katika uendeshaji wa kikao hicho na kurejea kufuta kauli zake mara kwa mara baada ya kuzidiwa presha na madiwani wake na kusababisha baadhi yao kuanza kutukana wazi wazi kikaoni.

Mmoja wa madiwani akiwa keshajaa presha akilalamikia maamuzi ya kikao hicho

Mh huyu aliamua kuporomosha matusi kwa Dc na meza yake baada ya kubaini kuwa hoja zake zilikuwa zinapuuzwa  baada ya kuhoji uhalali wa kikao hicho kutokuwa na mwitishaji ama theruthi mbili ya wajumbe kutosaini kuomba kiitishwe, hoja ambazo zilifutiliwa mbali hatua ambayo ilimfanya aanze kushambulia kikaoni hapo bila kujali miongozo na kanuni

Ikalazimu vijana wa jeshi la MWEMA wakae karibu na miembe chai yao kusubiria kitakachotokeza

Wandishi wakamweka kiti moto Dc kwanini alisoma barua ya chama kwenye kikao cha madiwani, yeye ni nani katika kikao hicho na wajibu wake ni upi?  katika maelezo yake mkuu huyo wa wilaya alisema hajafanya kosa lolote kwakuwa alisoma mapendekezo yaliyotolewa na chama cha mapinduzi kama mmoja wa wadau wa wilaya hiyo kama ilivyo kwa makundi mengine ambayo hakuyataja.


TAARIFA KAMILI YA TUKIO HILI ITAWAJIA IKIAMBATANA NA SAUTI ZA MALUMBANO KIKAONI, STAY TUNED