Sep 18, 2011

SHIRIKA LA ELIMISHA TANZANIA MKOANI MBEYA LAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA

Shirika lisilo la kiserikali la Elimisha Tanzania lenye makao yake makuu mkoani Mbeya, jana limeanza utekelezaji wa mradi wake wa kujenga uwezo kwa wanachama wa asasi hiyo katika masuala ya usimamizi, uendeshaji na utawala ikiwa ni hatua ya kujiimarisha katika utoaji huduma kwa wananchi wake.
Mafunzo hayo ni matokeo ya ruzuku ambayo shirika limepata kutoka The Foundation for Civil Society kwaajili ya kujengea uwezo mashirika ya kiraia katika kutekeleza majukumu yake, ambapo shirika hilo ni miongoni mwa asasi chache zilizonufaika na ufadhiri huo.
Mkurugenzi wa shirika hilo Festo Sikagonamo anasema,hatua hiyo ni ya msingi katika safari ndefu ya kuwafikia watanzania katika malengo ya muda mrefu, ambapo shirika linakusudia kutekeleza program zinazolenga katika kuinua kipato kwa makundi maalumu ya jamii, kufanya tafiti kwaa kushirikiana na wanahabari, kutandaa na kuimarisha uwezo wa asasi yenyewe.
anaeleza kuwa wiki ijayo shirika litakuwa kwenye hatua nyingine ya kutengeneza mpango mkakati wake  ambao utaongoza shirika kwa kipindi cha miaka mitatu na kwamba kupitia mpango kazi huo, program kadhaa za maendeleo zitatokana na mtazamo utakaojengwa kwa kushirikisha wadau mbalimbali mkoani humo.
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Bwana Kunzugala kutoka Tanzania Chamber of Commerce akiwezesha mafunzo hayo

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo

Kuna wakati washiriki walipata fulsa ya kufanya ,mawasilisho kwa vikundi namna ya kutengeneza sheria ndogo ndogo za uongozaji shirika

Hali ya mawasilisho iliendelea kujenga uwezo kwa wanachama kujiamini bila kujali jinsi

Msisitizo ulimaanisha asasi ijipange kuwa kioo katika jamii ya mbeya katika kuwafikia watu wengi kwa ubora lakini pia huku ikijitahidi kutafuta wadau wa kushirikiana nayo. TAYARI ASASI YA ELIMISHA IMESHATEKELEZA MRADI WA KUFANYA UTAFITI WA UWEZO WA WATOTO WALIO UMRI WA KWENDA SHULE MIAKA 7 HADI 15 KUSOMA, KUHESABU NA KUANDIKA KATIKA WILAYA ZA ILEJE, KYELA NA MBARALI KWA KUSHIRIKIANA NA MTANDAO WA ELIMU TANZANIA TENMET KUPTIA PROGRAM YA UWEZO.