Oct 11, 2011

MWANAMZIKI ALIYETUNGA DONT KUBEBA ZAMBIA ATAKA SATA AMKUMBUKE


Dandy Krazy al maarufu kama ZED
LINK YA WIMBO HAPO JUU
na Danny Tweve  -Lusaka
Mwanamziki Dandy Krazy wa nchini Zambia Maarufu kama ZED ambaye hivi karibu wimbo wake wa Don’t kubeba(donch kubeba) ukimaanisha tunza siri! Ameibuka akimtaka rais mpya Michael Sata ampe madaraka kwakuwa wimbo wake ulifanya kampeni zilizomwezesha kuingia madarakani.
Akizungumza katika moja ya taarifa za Televisheni ya nchini humo ya Muvi, Kratzy amesema wimbo huo ambao ulitumika kama slogan ya chama cha Patriotic Front ulikuwa ujumbe mhimu katika mafanikio ya rais Sata baada ya kutumika katika kipindi chote cha kampeni.
Mmoja wa wanaharakati nchini Zambia ambaye pia ni mwandishi wa habari Henry Kabwe, serikali ya Zambia imelichukulia jambo hilo kama kitu cha kawaida, ingawa mwanamziki huyo bado ameendelea kusisitiza kuwa anategemea kudra za rais kumpa madaraka katika teuzi zake zinazoendelea.
ZED anatumia msemo huo ambao rais Satta alikuwa akisisitiza wakati wa kampeni za kimya kimya kabla ya kutangaza nia yake ya kugombea urais kwa mara ya kwanza baada ya kuacha kazi kwenye shirika la Reli la Uingereza .
Kutokana na madai hayo ya ZED wananchi wa Zambia wamekuwa nyuma yake wakieleza kuwa mwanamziki huyo alijitoa moja kwamoja na kuonyesha wazi kutunga nyimbo za kumpamba Sata na kwamba hatua yake ya kudai ujira wa madaraka ni muhimu iungwe mkono
Staili ya wimbo huo inachezwa kama kiduku kwa mapaja kutawanyika na baadaye kukutanishwa, imekuwa maarufu nchini Zambia na wimbo huo umekuwa ukipigwa  kwenye maduka ya kanda na yale ya kawaida licha ya kampeni na uchaguzi kwisha.
Donch kubeba imemfanya ZED kuwa adui wa chama cha MMD ambacho kilikuwa kimemsimamisha mgombea wake kwa mara ya pili Rupia Banda.
Kwa ujumla mali zilizokuwa zikimilikiwa na chama hicho ambazo zilitokana na michango ya wananchi zimenyang’anywa na serikali ya sata ikiwa ni pamoja na michango iliyokuwa ikichukuliwa kwenye masoko na ushuru mwingine.