Oct 16, 2011

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATEMBELEA MABANDA KABLA YA UZINDUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KESHO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akikaribishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh. Rajabu Rutengwe, wakati alipowasili katika vinwaja vya maonyesho ya biashara na kukagua mabanda kwenye viwanja vya Idara ya Maji mjini Mpanda, kabla ya kongamano la Owekwzaji katika ukanda wa mkoa ya kanda ya ziwa Tanganyika. Mkioa hiyo ni Rukwa, Kigoma na Katavi, Mtandao wako wa Umma FULLSHANGWEBLOG upo eneo la tukio na unakuletea matukio hayo moja kwa moja kutoka mjini Mpanda.
Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Dk. Jakaya Kikwete, utakaofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini Mpanda kesho Oktoba 17/ 2011 na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali, wakiwemo wawekezaji wa ndani na wa nje ya Tanzania.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho ya biashara katika viwanja vya Idara ya maji mjini Mpanda, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Injini Stella Manyanya.
Waziri Mku Mizengo Pinda akitembelea banda la mkoa wa Rukwa katika maonyesho hayo.
Waziri Mku Mizengo Pinda akitembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia ngoma ya kabila la wafipa kutoka mkoani humo, wakati kikundi cha ngoma kilipokuwa kikitumbuiza.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata Maelezo ya mipango mikakati ya Mkoa wa Kigoma katika banda la mkoa huo, kutoka kwa maofisa wa mkoa huo Bw. Ballonzzi Steven Rutta kulia.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwassa kulia akizungumza na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya Waziri Mkuu kuzungumza na waandishi wa habari, kushoto ni Chrisant Mzindakaya ambaye amewahi kuwa mbunge kwa muda mrefu, mmoja wa waekezaji wazawa mkoani Rukwa na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injini Stella Manyanya.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimtania Monica Maduka msanii wa ngoma ya kabila la Kisukuma mara, baada ya kumaliza kucheza ngoma yao katika maonyesho hayo, Waziri Mkuu alionekana kufurahishwa sana na ngoma za utamaduni za kikundi hicho.
Waziri Mkuu akipata maelezo kutoka kwa Emmanuel Peter ambaye ni Mining Technician wa Kampuni ya Katavi & Kafumu Mining, wakati wa ziri mkuu alipotembelea banda la kampuni hiyo wengine, ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.