Nov 1, 2011

DC Mabiti Aamuru Wachimbaji Dhahabu Waondoke

Mkuu wa wilaya Singida Paschal Mabiti akizungumza na wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu kijiji cha Sambaru wilayani humo, ambapo aliwapa siku tatu hadi ijumaa wiki hii kuhakikisha wameondoka kwenye eneo hilo ili kumpisha mwekezaji kampuni ya Shanta.
Mchimbaji George Stiven,kwa niaba ya wenzake akiomba waongezewe muda ili waondoke kwenye eneo hilo kama ilivyoamuliwa na serikali kwa ajili ya kumpisha mwekezaji anayetarajia kufungua mgodi,baada ya kukamilisha kazi ya kutafiti madini ya dhahabu.
Baadhi ya askari kikosi cha kutuliza ghasia waliofuatana na mkuu wa wilaya ya Singida Paschal Mabiti, wakiwa kwenye eneo la mkutano, tayari kudhibiti lolote linaloweza kuhatarisha uvunjifu wa amani
Singida
Novemba 01,2011
MKUU wa wilaya Singida Paschal mabiti ametoa siku kwa wachimbaji wadogo wanaofanya kazi zao kwenye kijiji cha Sambaru, kuondoka, haraka, bada ya hapo watakumbana na nguvu ya dola.
Mabiti amesema eneo hilo linalotoa madini ya dhahabu ni halali kwa mgodi wa kampuni ya Shanta, iliyotafiti na kupata kibali kwa kazi hiyo.
Alitoa karipio hilo juzi jumatatu, wakati akizungumza na wachimbaji hao katika viwanja vya kambi namba moja, kijijini Sambaru.
Alisema Shanta inayo leseni halali ya kutafiti na kuchimba dhahabu katika maeneo hayo, na amekamilisha maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kuanza kazi ya mgodi.
“Tumezungumza sana na ninyi,tena mara nyingi sana na mazungumuzo hayo, nimekuwa nawaeleza kuwa, Shanta amewapa ruhusa kuchimba madini katika eneo hili kwa muda tu, Sasa muda huo umekwisha, mnatakiwa kuondoka kwa hiari yenu,”alisema.
Baadhi ya wachimbaji waliomba kuongezewa muda ili wahame eneohilo.
Huku wengine wakisema wazi hawapo tayari kuona wanaporwa maeneo yao, hivyo wameiomba serikali kuingilia kati malalamiko yao waliyodai sasa ni ya muda mrefu.
Walitoa tahadhari kupatikana suluhu, ili yaliyotokea mkoani Mara na Shinyanga yasijirudie mkoani Singida.
Na Elisante John