Nov 30, 2011

WANA RUVUMA, RUKWA NA KATAVI WAITEMBELEA MAKUMBUSHO NA NYUMBA YA UTAMADUNI DAR ES SALAAM

Mkuu wa mkowa wa Rukwa Mh Eng Stella Manyanya (MB) (alie simama) akimsikiliza kwamakini Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Dkt Pual Msemwa, wengine ni wanakikundi wa Ngoma kutoka Ruvuma walio kuja kuhudhuria Tamasha la watani zao la Jamii ya watu wa Rukwa na Katavi lililo fanyika Kijiji cha Makumbusho hivi karibuni.
Watani wa Wangoni jamii ya watu wa Rukwa na Katavi nao walipata wasaa wakuitembelea makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaama. Hapa wakiangalia magari ya Kihistoria.
Wanakikundi wa ngoma toka Mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza kwa makini mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni juu ya Mwenge Uliopandishwa mlima wa Kilimanjaro miaka ya 60.
Chifu Emanuel Zulu Nkosi wa Wangoni na wanakikundi cha Ngoma cha mkoa wa Ruvuma wakipata maelezo toka kwa Mama Shayo walipo tembelea makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Dkt Paul Mswemwa akiwakaribisha wanajamii wa Rukwa na Katavi walipo wasili makumbusho hapo.
Kikundi cha Ngoma kutoka Ruvuma kikiwa katika picha ya pamoja na Chifu wa Wangoni alie shika mtoto katikati. kutoka swahili villa