Nov 20, 2011

Waumini wamkataa askofu, wamzuia asiingie kanisani

Askofu JOHN DAUDI LUPAA katikati akitoka (mwenye koti la Bluu) kituoni kuripoti kuwa amezuiwa kuingia katika kanisa
Askofu JOHN DAUDI LUPAA akiwa amepozi mara baada ya kuzuiwa kuingia kanisani
Waandishi wa habari ambao alikuja nao pia walishikwa na mshangao mara baada ya kukuta hali ni tofauti na alivyowaeleza.
Waumini wakimaliza ibada yao kwa amani pasipo uwepo wa askofu

Kabla ya askofu JOHN DAUDI LUPAA wa kanisa la Anglikana Jimbo la Rift Valley kuzuiwa na waumini wa kanisa lake hii leo asiingie kanisani, hivi karibuni waumini wa kanisa la Kilimatinde mkoani Singida walibandika mabango katika kuta za kanisa wakimkataa mchungaji wa mtaa na Askofu, huku wakitoa hoja kadhaa za kuukataa uongozi huo, baadhi ya hoja walizotoa ni kama ifuatavyo

  1. Fedha za mnara wa Tigo ambao upo eneo la kanisa hilo.
  2. Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya matengenezo ya gari la wagonjwa ambazo zimetumika kinyume utaratibu.
  3. Kesi nyingi zenye hasara kwa Jimbo la Rift Valley
  4. kufukuza wafanyakazi kwa maslahi yake binafsi
  5. kumng'ang'ania Mkuu wa Chuo cha Uuguzi kwa maslahi yake binafsi,wanafunzi kuchangia shilingi elfu 50000 kwa kila mwanafunzi lakini fedha hizo hazijulikana nini zinafanya huku pia wakristo wa Jimbo la Rift Valley wakichangia shilingi 2oo.ooo kila Parish kwa ajili ya ukarabati wa Chuo cha Unesi hata hivy kazi ya fedha hiyo haijaonekana.
  1. Dai lingine ni kupuuza malalamiko ya wakristo wa jimbo hilo.

Barua hiyo aliandikiwa na waumini wa kanisa hilo na kutumwa kwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana ,Katibu mkuu na Msajili wa jimbo na nakala kupelekwa kwa Askofu wa Dayosisi ya Rift Valley John Lupaa anayetuhumiwa na waumini hao, Mchungaji wa mtaa Samuel Chilewa ,OCD wa Manyoni na OCS Kilimatinde.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza waumini wawili walitengwa na mchungaji wa kanisa hilo kutokana na wao wanachokieleza kuwa ni kwenda kuhoji kuhusu fedha za mnara wa Tigo uliopo katika eneo la kanisa . Lakini pia mara baada ya kutaka kumrudisha muumini mmojawapo kanisani kati ya wale waliotengwa na kanisa , walimwita na kufanya makubaliano ya maneno ya kutamka wakati kurudi kund kundini.

Hivyo aliombwa kukubali kile wanachomuelekeza ili akatamke mbele ya kanisa lakini tofauti na alivyoelekezwa akajikuta anazungumza mbele ya watu tofauti na walivyokubaliana kabla ya siku ya ibada.

Kabla ya kuibuka kwa mgogoro huo pia kanisa la Kintinku ambalo liko chini ya dayosisi ya Rift Valley ambayo inaongozwa na askofu huyo, nako uliibuka mjadala wa kumkataa askofu huyo.

Hivi juzi pia waumini hao waliandika barua kwa askofu Mkuu kuwa WAMEJITOA katika utawala wa askofu huyo, hivyo kila mali ya kanisa itakuwa chini yao mpaka pale atakapojiuzulu.