Nov 18, 2011

WAZIRI WA FEDHA MSTAFA MKULLO AWEKA JIWE LA MSINGI KIKWALUZA ANGA CHA HAZINA NDOGO DODOMA

Mh Waziri Mkullo akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuweka jiwe la msingi la Jengo la Ghorofa la hazina Ndogo Dodoma ambalo litasidia pia shughuli za wizara wakati wa Bajeti, Mchina aliyeko mbele ni Mkurugenzi Mtendaji  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Group  SIX  International LTD inayojenga jengo hilo.

Mh Mkullo akifurahia jambo kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Nchimbi

Utadhani anaanzisha pambio vile, hapana ni furaha iliyoje baada ya kuahidiwa kuwa jengo hilo litakabidhiwa miezi miwili kabla ya muda uliopangwa kutokana na kasi ya ujenzi inayofanya na kampuni ya Group Six International Ltd ya China

Naomba nisisitize, muda mrefu serikali inalaumiwa kutokana na utendaji wa baadhi yenu ninyi watumishi hasa katika uchelewesha wa mafao ya wazee, ubadhirifu na rushwa, naomba nieleze wazi katika hili tutahangaika na watu, kwakuwa tumeshatoa mafunzo kwa watendaji wetu sasa tunaamini atakayefanya makosa kama haya atakuwa kanuwia na siyo bahatimbaya tena.


Akiweka jiwe la msingi

Baadhi ya maafisa wa wizara na hazina waliohudhulia kwenye hafla hiyo

Waziri Mkullo akihutubia kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la Hazina Dodoma  picha zote na Indaba blog

Hiki ndiyo kikwangua anga cha hazina ndogo Dodoma kinachojengwa karibu na chuo kikuu cha DODOMA ambapo kulingana na Mhasibu Mkuu wa serikali  kitagharimu jumla ya shilingi  16,849,136,419 kama huwezi kusoma hiyo tamka Bilion 16 milion 849 laki moja na elfu thelathini na sita na mia nne kumi na tisa tu!!!!!!

Namna hii Dodoma inaelekea kutimia ile ndoto ya makao makuu ambapo shughuli za serikali zitahamia huko

Hii ndiyo sura ya Mbele kama kamera ya Indaba ilivyoweza kunasa

Picha ya pamoja nje ya jengo hilo litakalokamilishwa August mwakani, lakini kulingana na kasi yake yawezekana likakamilika mwezi June, 2012  yaani miezi miwili kabla ya muda wa kukabidhi uliomo kwenye mkataba/

Uongozi wa Chuo cha Mipango pia umeshiriki katika tukio hilo, kwani ni miongoni mwa vyuo vilivyo chini ya wizara  ya Fedha Mipango na Uwezeshaji Picha na Danny Tweve wa Indaba blog.