Dec 2, 2011

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA CUF IKULU JIJINI DAR LEO

Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CUF,Mh. Machano Khamis Ally ambaye ni Kiongozi wa Ujumbe na uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) uliofika Ikulu jijini Dar es salaam leo Kuonana na kuzungumza na Rais Kikwete juu ya Sheria ya kuanza kwa mchakato wa kutafuta Katiba Mpya.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Ntatilo.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Mh. Mnyaa Mohamed Habib
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mh. Ismail Jusa.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa kwenye Mazungumzo na Ujumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) uliofika Ikulu jijini Dar es salaam leo kuzungumzia Sheria ya kuanza kwa mchakato wa kutafuta Katiba Mpya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa serikali yake umekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Machano Khamis Ally kuhusu namna ya kuboresha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.
Mkutano huo umefanyika asubuhi ya leo, Ijumaa, Desemba 2, 2011, Ikulu, mjini Dar es Salaam na ujumbe wa CUF umemkabidhi Mheshimiwa Rais mapendekezo ya chama hicho kuhusu namna Sheria hiyo inavyoweza kuboreshwa.
Baada ya majadiliano ya saa mbili, pande hizo mbili zimekubaliana kujipa nafasi ya kutafakari zaidi na zitakutana tena jioni ya leo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
02 Desemba, 2011