Mtumishi Anthony Lusekelo |
† Asema Mvua ni Baraka na sio mpango wa Mungu Mvua kunyesha na kuua watu.
† Asema Watu wamezoea kusoma tu kwenye Biblia Kuwa Mungu alisimamisha Jua, Mungu alitawanya Bahari sasa nasema hiyo mvua haitonyesha.
† A sema endapo Mvua zitanyesha leo jijni Dar es salaam na kisha zikaleta madhara basi atajiuzulu uchungaji
Mtumishi Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana usiku kupitia Kituo cha Television cha Chanel Ten aliwaambia watanzania hususani waishio Dar es salaam kwamba pamoja na Idara ya hali ya hewa nchini kutangaza kuwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo alhamisi 29-31/12/2011 mvua kubwa zitanyesha jijini Dar es salaam na sehemu zingine za nchi, mvua hizo hazitareta madhara kama ilivyotokea siku chache zilizopita ambapo mvua hizo zilisababisha mafuriko kwa wakazi wa mabodeni jijini Dar es salaam na kupelekea vifo vya watu zaidi ya Arobaini.
Mtumishi Lusekelo alisema” Mvua ni Baraka na sio mpango wa Mungu Mvua kunyesha na kuua watu, Mimi Anthony Lusekelo nina nguvu kuliko hiyo mvua na kama itanyesha Haitokuwana na madhara”. Aliendelea kusema kuwa “Mimi kama mtumishi wa Mungu hiyo mvua haitonyesha na watu wamezoea kusoma tu kwenye Biblia Kuwa Mungu alisimamisha Jua, Mungu alitawanya Bahari sasa nasema hiyo mvua haitonyesha, naweza leta mvua naweza sitisha mvua nmeshakaa kwenye magoti”.
Katika hali ya kuonyesha msisitizo juu ya kauli yake Mchungaji Lusekelo alienda mbali zaidi na kusema endapo Mvua zitanyesha leo jijni Dar es salaam na kisha zikaleta madhara basi atajiuzulu uchungaji. Akaendelea kusema kuwa na wale wote ambao huwa hawaamini mambo ya Mungu na waamini baada ya mvua kutonyesha siku ya leo. Mtumishi Lusekelo alisema wakati mvua ziliponyesha na kuleta madhara yeye hakuwepo jijini Dar es salaam.
Mtumishi Lusekelo awali kabla hajaanza kuwaambia mamilioni ya watanzania juu ya AGANO lake hilo na MUNGU, alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu maoni yake katika miaka Hamsini ya Uhuru. Alisema Pamoja na changamoto tulizonazo kama watanzania, bado kuna Mengi ya Kujivunia kwa hapa Mungu alipotufikisha.