Apr 26, 2012

UZINDUZI WA JENGO LA KITEGA UCHUMI WA KIJITONYAMA LUTHERAN CENTRE (KLC) KUFANYIKA JUMAPILI TAREHE 29/04/2012

KUTOKA BLOG YA MICHUZI
Katibu wa baraza la kanisa hilo Dkt. Victoria Kayombe (kushoto) akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi wa Jengo la Kijitonya Lutheran Centre (KLC) litakalotumika kama kitegauchumi kwa Kanisa hilo,Jengo hilo litazinduliwa rasmi Aprili 29.katikati ni Mchungaji wa Usharika wa Kijitonyama Ernest Kadiva na Kulia ni Mwenyekiti wa ujenzi Bw.Sanyiel Kishimbo.
Mchungaji wa usharika wa kijitonyama,Ernest Kadiva akifafanua jambo kwa wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la kitegauchumi cha usharika huo litakalojulikana kama KIJITONYAMA LUTHERAN CENTRE (KLC) litakalozinduliwa jumapili tarehe 29 mwezi huu,Ujenzi wa jengo hilo ulianza mwaka 2009 na kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 3.5.
Mchungaji wa Usharika wa Kijitonyama,Ernest Kadiva (kushoto) akibadilishana mawazo na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre (KLC) katikati Katibu wa baraza la kanisa hilo Dkt. Victoria Kayombe na Mzee wa baraza la kanisa, Leonard Shayo wakati walipokutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwafahamisha juu ya uzinduzi wa jengo hilo utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu.
Katibu wa baraza la kanisa hilo Dkt.Victoria Kayombe akiongea na baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre (KLC) litakalotumika kama kitega uchumi kwa kanisa hilo,mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa jengo hilo utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu,wa pili kutoka kushoto ni Mchunga wa Usharika wa Kijitonyama Ernest Kadiva,Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi Selina Mkony,Mzee wa baraza la kanisa Leonard Shayo na Mjumbe wa kamati hiyo Peniel Uliwa.Ujenzi huo umegharimu kiasi cha Bilioni 3.5.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Dayosisi ya Usharika wa Kijitonyama Dkt. Hans Macha (kulia) akisisitiza jambo kwa Katibu wa Kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre (KLC) Bw.Leonard Shayo ambalo litatumika kama kitega uchumi wa kanisa hilo,Baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwafahamisha juu ya uzinduzi wa jengo hilo utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu.
Baadhi ya waumini na wanakamati wa maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre(KLC)walioudhuria kwenye mkutano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya uzinduzi wa Jengo hilo litakalozinduliwa Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre (KLC) kama linavyoonekana pichani litakalozinduliwa tarehe 29 mwezi huu,Jengo hili litatumika kama kitega uchumi wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki ya Pwani.