Apr 25, 2012

WAMI DAKAWA MAISHA YANAKWENDA , MATUMAINI YA WANANCHI KUJILETEA MAENDELEO BADO NI MAKUBWA

Hii ni moja ya kaya za wafugaji katika kijiji cha Wami Dakawa kwenye kitongoji cha Makuture wakati timu ya wanachuo wa chuo cha Mipango kozi ya stashahada ya uzamili walipopiga kambi katika kuandaa mpango wa uwiano wa manedeleo kijijini hapo

Mambo safi mapumziko muhimu nyakati za mchana

Kijiji cha Wami Dakawa kilibadilika na kuwa taasisi ama kituo cha teknolojia kutokana na wanakijiji na watoto kufika kuangalia zana za kufanyia kazi zilizoletwa na wanachuo wakati wa utafiti wao, angalau kilamwanachuo alikuwa na kitendea kazi chake ( kinakirishi) al maarufu kama laptop

hatimaye baada ya kumaliza shughuli hiyo tuliamua kupiga picha ya pamoja , katikati mwenye nyekundu ni Dr Nhembo ambaye ni mkufunzi mwandamizi wa chuo cha Mipango Dodoma na pia  mtaalamu wa mipango ya Mikoa na mazingira.