May 1, 2012

ATI SERIKALI INA UBIA NA WALA RUSHWA

Risala ya vyama vya wafanyakazi mkoani DODOMA imeituhumu serikali kuwa ina ubia na wala rushwa na ndiyo sababu imekuwa ikifumbia macho kushuhulikia kero hizo,
wakisoma mbele ya mkuu wa mkoa wa Dodoma wafanyakazi mkoa wa Mbeya wameonyesha hofu yao kuwa kufanya hivyo kumekuwa kukiwakatisha tamaa.
more  sooon

MEI MOSI DODOMA YAANZA VYEMA MAANDAMANO YAMALIZIKA

Wafanyakazi wakiendelea na maandamano kuelekea uwanja wa Jamhuri Mjini DODOMA mchana huu

Taasisi na Idara mbalmbali zikiandamaana  katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi MEI MOSI

Chuo cha Biashara Dodoma CBE wakiwa miongoni mwa waandamanaji wakipita mbele ya mgeni rasmi

WIMBO wa solidarity forever ukiimbwa kwenye maadhimisho hayo

Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki maadhimisho hayo wakifuatilia kwa makini maonyesho ya taasisi mbalimbali wakati magari na mbwembwe hizo zikipitishwa kwenye uwanja wa jamhuri

Sehemu ya waaandamanaji wakieelekea kwenye jukwaaa kuu ambako mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi alikuwa mgeni rasmi

Wafanyakazi wa manispaa ya Dodoma wakifanya usafi  kwenye uwanja wa hamhuri kama sehemu ya maonyesho ya maadhimisho ya siku ya wawafanykazi mei mosi

Wafanyakazi wakifuatilia mbwembwe za maonyesho ya taasisi mbalimbali yaliyokuwa yakipita kwenye jukwaa kuu

Baadhi ya wafanyakazi bora wakisubiri muda mwafaka wa kuchukua chao mbele ya mgeni rasmi

MEI MOSI DODOMA KUMEKUCHA ASUBUHI

  
Ndivyo sanamu ya mwalimu Nyerere ikionyesha kulinyoshea mkono jengo la chamacha Mapinduzi katika mji wa DODOMA ambapo asubuhi wafanyakazi wanaandamana kuelekea viwanja vya Jamhuri kwaajili ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi.
Hawa ni watu muhimu katika kuifanya miji yetu ilingane na hadhi zake, hapa wakiwa na zana zao katika maandalizi ya maandamano katika viwanja vya  Nyerere Square
  

Hapa ni waahadhiri wa chuo cha Mipango DODOMA wakibadilishana mawazo wakati wa maandalizi ya maandamano katika viwanja vya Nyerere square mjini DODOMA
  

Profesa Zilihona akizungumza na wahadhiri wengine wa chuo cha Mipango, anayeonekana kuchangia hapo ni Dr Malila, kulia  ni Bwana Haule afisa Habari na mawasiliano Chuo cha Mipango Dodoma
  

Ni katika kuhanikiza sherehe za Mi Mosi mjini Dodoma, chuo cha Mipango chajiakisi namna kinavyokabili changamoto za ajira kwa wahitimu wake
  

 

Mdau wangu wa siku nyingi toka tupoteane, Dr Ngumbi katikati akiwa na wafanyakazi wenzake wa halmashauri ya wilaya ya wilaya ya Mpwapwa katika viwanja vya Nyerere
  

Ni katika mazingira ya maandalizi ya maandamano hapa Nyerere square Dodoma endelea kuwa nasi tukufahamishe yanayojiri