Oct 12, 2012

ABBAS KANDORO AONYA WATAALAMU WA KILIMO KUFANYA KAZI KWA MAZOEA


MKUU wa Mkoa wa Mbeya Bw.Abbas Kandoro amewaonya wataalamu wa kilimo kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kukaa maofisini badala ya kwenda mashambani waliko wakulima na ili waweze kusaidiana wakulima kujua mbinu za bora za kuboresha mazao yao kuliko kuendelea kufanya kazi za kilimo bila wataalamu kilimo kuwepo .

Mwandishi wetu Esther Macha anaripoti kutoka Mbeya kuwa Bw. Kandsoro alisema wataalamu wa kilimo wanapaswa kuwa karibu na wakulima wao waliopo vijijini kuliko mazoea yaliyojengeka miongonbi mwao yao ya kukaa maofisini kusubiri taarifa za kilimo wakati taaluma yao inawataka kufika mashambani waliko wakulima wenyewe.

 Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo baada ya kupewa taarifa ya idara ya kilimo ya halmashauri ya wilaya ya Mbeya alipofanya ziara na ndipo akakutana na madudu kama aliyosikia kwenye tarifa ya wilaya ya Mbozi na kuikataa.

 Alisema hatua iliyopo kwa wataalamu kutokuwa karibu na wakulima ndiyo chanzo kikubwa cha wachuuzi kupata fursa ya kwenda majumbani kwa wakulima na kununua mazo kisha wanaondoka nayo pasipo hata kulipa ushuru.


Bw. Kandoro alisema madudu hayo ni pamoja na kuwepo kwa takwimu zinazoonyesha taarifa za makadirio ya mavuno ya nafaka hali iliyoashiria mavuno bado yanaendelea ama hayajafanyika wakati umekwisha hivyo kulipaswa kuwepo takwimu sahihi na si matarajio tena.

“Ndugu zangu hatuwezi kwenda katika utaratibu kama huu haiwezekani kabisa.Unasema shughuli zinaendelea! Wapi wanaendelea kuvuna mpaka leo hii?.Hivi unajua tayari tuko katika msimu mwingine wa kilimo?” alihoji Bw.Kandoro.

“Kwa nini mnafanya kazi ya kukokotoa takwimu mkiwa maofisini?Na hili nimeliona mahala pengi eneo la kilimo lin a ubabaishaji mkubwa.Mabwanashamba wapo lakini kila kukicha wanacheza na takwimu maofisini.Vijijini waliko wakulima hawaonekani”


Alisisitiza kuwa  utaratibu maalumu wa ukusanyaji takwimu zinazohusiana na kilimo ikiwemo kupeleka maaofisa takwimu katika magulio ili waweze kujua ni kiasi gani cha mazao kinauzwa.

KUTOKA FRANCIS GODWIN BLOG