Nov 11, 2012

Msaidizi wa askofu wa KKKT Dayosisi ya Konde Mchungaji Geofrey Mwakihaba akitamka neno la baraka kabla ya kuuweka mche wa mparachihi  kwenye shimo tayari kuupanda ikiwa ni hatua ya kuzingua program ya sharika, majimbo na taasisi za Kilutheri kwenye Dayosisi hiyo katika upandaji wa miti kama sehemu ya hifadhi ya mazingira.


Msaidizi wa askofu  mchungaji Mwakihaba akipanda mche wa mparachichi kwenye kituo cha watoto kinachoendelea kujengwa kwenye usharika wa Vwawa

Mkuu wa Jimbo la Magharibi Mch. Mwambola akizungumzia uendelezaji wa program ya hifadhi mazingira kwenye sharika za jimbo hilo


Mwanafunzi wa  kipaimara  akipanda mti kama sehemu ya uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Makanisani na kwa waumini lililoanza msimu huu kwa KKKT dayosisi ya Konde

Pia familia ya Danny Tweve imeshiriki kwenye ibada  hiyo ikikumbuka miaka minne iliyopita ambapo Mch Mwakihaba ambaye alifungisha ndoa hiyo hapakuwa na matunda haya kwa mtoto wa kiume  na aliyebebwa 


Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Konde, imetoa maelekezo kwenye majimbo na sharika zake kujielekeza katika utekelezaji wa mipango ya kuhifadhi mazingira ili kuepusha  madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na kushindwa kutawala vyema mazingira kwenye maeneo yao.
Akizungumza kwenye ibada ya Kipaimara  katika usharika wa  Vwawa wilayani Mbozi Msaidizi wa Askofu Mch. GEOFREY MWAKIHABA amesema utaratibu uliobuniwa na uongozi wa jimbo la Magharibi utasaidia kuwakumbusha waumini na wananchi kwa ujumla juu ya uhifadhi wa mazingira
Amesema jimbo hilo limeanzisha utaratibu wa kupanda miti kila msimu wa mvua unapoanza na kwamba kanisa linatumia fulsa ya ibada maalumu kama za kipaimara na ubatizo kwenye nyakati hizo kuzindua kampeni za upandaji miti  kama kanisa, na waumini wake.
Amefafanua kuwa hatua hiyo pia itasaidia watoto kujihusisha zaidi na shughuli za kutunza mazingira kutokana na kuandaliwa katika malezi yao wakijua umuhimu wa raslimali rafiki za mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wake