Jan 27, 2013

BARAZA LA MADIWANI MBOZI LAGAWA MALI NA WATUMISHI , UKIMYA WATAWALA WAKATI WA KUTANGAZA WANAOENDA KUANZISHA WILAYA M


Mwenyekiti akiwapiga dongo watumishi kuwa wasije mnunia ati alikuwa anasoma kwa msisitizo majina yao na akaamua kutoyasoma na badala yake kutaja tu idadi ya wanaoenda momba kwa kila idara
Mwenyekti CCM Mbozi Mzee Aloyce Mdalavuma akizungumza kwenye mkutano huo

baadhi ya wakuu wa idara wakifuatilia majadiliano hayo
Mkurugenzi Mbozi akizungumza kabla ya kuanza kupitia mali zinazogawanywa


Watumishi wakimeza mate kwa shida wakati wakisubiria orodha ya wanaoenda kuanzisha wilaya mpya ambayo hata hivyo majina hayakusomwa hadharani

Madiwani wakifuatilia mjadala
Mkuu wa wilaya ya Momba  Abiud Saidea akizungumza kwenye mkutano huo
Orodha ya magari yaliyogawanywa kwenye mchakato huo ambapo Momba wamepewa magari 17
Mbunge wa Mbozi Mh Zambi akizunguma kwenye kikao hicho ambapo alisisitiza maslahi ya wananchi yaangaliwe zaidi kuliko ubinafsi wa madiwani wenyewe

Kabla ya kuingia ukumbini wajumbe walilishana yamini na makubaliano ya kusimamia na kutetea hoja walizokubaliana kabla ya kikao
Mwenyekiti halmashauri akifungua baraza hilo

Dua ilitangulizwa kwenye kikao hicho ili kuwaongoza madiwani kutawaliwa na busara na hekima
Waraka kutoka TAMISEMI ukisomwa kwenye kikao cha baraza la madiwani juu ya namna ya ugawaji mali na raslimali watumishi nk
Mwenyekiti wa CCM Momba bwana Juma Mwandusu akizungumza kwenye mkutano huo akielezea kuwa huo ni mwendelezo wa hatua nyingine zilizofanyika zikiwemo za kisiasa ambapo CCM katika uchaguzi wa mwaka jana walipata viongozi kwa wilaya zote Mbili
Mbunge wa Mbozi Magharibi Ernest Silinde akizungumzakwenye mkutano huo wa kugawa mali