Jan 18, 2013

BLACK LEOPARDS KUTOKA AFRIKA YA KUSINI YATUA DAR KUKIPIGA NA YANGA

Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili mchana wa leo kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa na Yanga ya Dar es Salaam, mchezo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini.
Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waratibu wa mchezo huos, kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Pichani kushoto ni Shaffih Dauda, Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga,Mtangazaji wa kipindi cha Sports Extra,Mbwiga Mbwiguke,Mdau Juma pamoja na Stuart
 Nahodha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili na kikosi chake kizima leo mchana tayari kwa kupambana na timu ya Yanga Sports Club,kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Waratibu kutoka Prime Time Promotions Ltd,Shaffih Dauda pamoja na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo Godfrey Kusaga wakifanya mawasiliano leo mchana mara timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini ilipowasili kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
 Shaffih Dauda akiwa ameambatana kocha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini,Abel Makhubele mara baada ya kuwasili leo mchana kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
 Wachezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiingia kwenye basi kubwa la timu ya Yanga,wayatarajia kumenyana nayo hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa,Jijini dar.
Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwasili mapema leo mchana kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Picha zote na JIACHIE