Jan 23, 2013

MAKETE NA MAZINGIRA YAKE YANAVYOVUTIA KWA VIUMBE MBALI MBALI

Hili ndilo eneo la Kitulo ambapo sasa ni miongoni mwa mbuga za wanyama zenye mvuto wa aina yake kutokana na kusheheni aina mbali mbali za maua  na ndege ambao hutua  mara moja katika kipindi cha mwaka mzima 

Hivi ndivyo makete inavyoonekana kwa mbali  katika baadhi ya vijiji 

Hii ni sura ya miongoni mwa vijiji vya wilaya ya Makete hapa ni Isapulano 

Bado Makete mazingira yake hayajaharibiwa na ikiwa wananchi wataendeleza ile mipango ya miaka mingi ya upandaji miti, hali ya misitu huenda ikarejea katika kipindi cha miaka michache ijayo

Wanyama hawa maarufu kama simbilisi hufugwa kwa wingi katika wilaya ya Makete na wanafaa kwa lishe ! wana sifa za kuzaliana sana hasa kwenye mazingira yenye moto  karibu(jikoni)

Hapa ni wilayani Makete na kwa mbali kinaonekana chuo kipya cha VETA MAKETE , wilaya ya Kazi ndiyo motto wa wilaya Makete

PICHA ZOTE KUTOKA KWA TITO NGAJILO WA MAKETE PLATFORM