Mwanamziki Alick Macheso akiwa na kundi lake katika moja ya ziara zake nchini Uingereza mwaka jana mwezi November (wa katikati shati lenye wekundu na jaketi jeusi)
sehemu ya Minjonjo ya Alick Macheso katika upigaji wake gitaa ambapo hutumia miguu yake kukung'uta kitu mpini!!!!! bongo nani anaweza?.
na Danny Tweve wa Indaba Blog kwa msaada wa website ya Alick Macheso na Zimbabwean Breaking News
Serikali ya Zimbabwe imesema
itatoa ulinzi kupitia jeshi lake la ulinzi ZNA wakati wa onyesho la wanamziki
watatu maarufu nchini humo ALICK MACHESO,SULUMAN CHIMBETU na JAH PRAYZAH .
Aidha jeshi hilo limeahidi
kuendea kutoa ulinzi kwa shughuli za wanamziki hao nchini mwao hatua ambayo
itafanya wanamziki hao kuwa wa kwanza kulindwa na jeshi la nchi katika shughuli
zao za kimziki .
Kwa watu wengine wanaweza kudhani
kuwa mtu maarufu nchini Zimbabwe kwa muziki wake ni Oliver Mtukudzi, lakini
hali siyo hiyo kwani Oliver Mtukudzi amebaki kuheshimika kama mzee aliyeiongoza
sanaa katika utunzi wa nyimbo za busara
Alick Macheso ndiye chaguo la
wazimbabwe wengi katika nyimbo zake alizotoa katika album zipatazo 18 katika
vipindi tofauti huko nyuma, mtindo wao wa upigaji vyombo kwa kasi (miziki ya
zamani ya kwenye santuri enzi hizo ikitoka Kenya na Zimbabwe kama mangerengere ndiyo staili
inayouza mziki nchini Zimbabwe .
Kwa mujibu wa Zimbabwean
Breacking News, wanamziki hao watatu watafanya show hiyo kwenye uzinduzi wa
mchezo wa ngao ya hisani kwaajili ya kuadhimisha mwaka wa Jeshi la Zimbabwe ZNA
, mchezo unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Rufaro kati ya Timu ya Jeshi hilo Black Rhinos na CAPS
united.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda
mkuu wa ZNA Luteni Generally Philip Valerio Sibanda , Brigedia Generali Howard
Matombo alisema wanamziki hao wamekuwa waaminifu kwa jeshi la Zimbabwe kutokana na ushiriki
wao wakati wote tangu kuanzishwa kwa michezo ya ngao ya hisani ya jeshi hilo
Alick Macheso ambaye hata mmiliki
wa mtandao wa Indaba blog ni shabiki wake kutokana nakujaza miziki yake
nyumbani anawika hivi sasa na albam yake ya Kwatakabva Mitunhu”aliyotoa Disemba
05, 2012 huku akiingiza mwanamziki mpya kwenye bendi yake Kochekera.
Hata hivyo katika ukurasa wa
website yake Macheso anawaomba mashabiki wake waendelee kumwombea mwanamziki
wake mpiga gitaa Luckie Yahwe Mayor Mumiriki ambaye alipata stroke na sasa
anapata matibabu na mazoezi
sehemu ya maneno yake ALICK MACHESO KWENYE MTANDAO WAKE jana!
Please continue to pray for my sub-rhythm
player, Luckie 'Yahwe Mayor' Mumiriki, who is still struggling to for muscle
healing, following the stroke he suffered. Luckie has been a core member of my
band for years, it's painful not to see him on stage doing what he does best.
With your prayers and support, we hope to have Luckie back doing what he does
best.