Feb 24, 2013

KAMATI MAALUMU YATEMBELEA KUKAGUA MAZINGIRA YA KUHAMISHIA WILAYA YA MOMBA

Kamati ya wakuu wa idara ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Momba wakitembelea kijiji cha Nkala kukagua makazi yanayopendekezwa kukodishwa kwaaajili ya watumishi wanaoanzisha halmashauri ya Momba
Hii inapendekezwa kuwa ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ambako DED ndimo atakamotumia
Afisa Utawala na Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Lulandala alikuwa miongoni mwa wanaotembelea eneo la Momba kwaajili ya kuona mazingira hayo ya makazi ikiwa yataweza kufaa kwaajili ya maisha ya watumishi wanaohamishiwa huko
Padre Mande akizungumza na Uongozi wa halmashauri ya Momba kulia kabisa ni Mwenyekiti wa Halmashauri Bernard Sichilonga, akifuatiwa katikati Makamu Mwenyekiti Credo Simwinga na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Juma Kitabuge  juu ya uwezekano wa kutumia jengo la Chekechea kwaaajili ya ofisi za idara mbalimbali za halmashauri hiyo ya Momba
Hapa ni Mjini Chitete ambako ndipo makao makuu ya wilaya ya Momba, wageni njoo wenyeji wapone nyuma ya Noaha jamaa akaamua kuuza kuku
Afisa Utumishi Momba bwana Mfugale akaamua kutumia ziara hiyo kuweka kumbukumbu kwenye daraja la kitep tep ambayo kwa eneo hilo ni madaraja muhimu katka kurahisisha mawasiliano baina ya vijiji na vijiji


 Wakiangalia shamba la ufuta katika moja ya vijiji vya kata ya chitete
 Nyumba mojawapo ambamo watumishi wanatarajiwa kupangishwa baada ya kuanza maisha katika halmashauri ya wilaya ya Momba

MIUNDOMBINU kwaajili ya watumishi wanaohamia ni ya aina hii, watu wanajiuliza wataanza anza vipi?
Hapa ndipo sokoni kariakoo kwa wilaya ya Momba! namaanisha soko kuu la bidhaa mbalimbali kwaajili ya mahitaji ya nyumbani
haya ndiyo majengo yanayopendekezwa kutmiwa na halmashauri ya wilaya Momba kwaajili ya ofisi za idara mbalimbali  ambayo awali yalijengwa kwaajili ya chekechea kupitia kanisa katoliki
PICHA ZOTE NA GODFREY MWAKITWANGE