Feb 14, 2013

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA MPAKA WA TUNDUMA NA KUBAINI MADUDU!

Kamati ya Bunge ya huduma za jamii ikiongozwa na mwenyekiti wake Magret Sita MB na makamu wake Augustin Ndugulile MB huku wakiwa wameongozana na wajumbe wake pamoja na Naibu waziri wa afya Dr Seif Rashid imebaini manyanya kama siyo madubwasha ya uuzaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku kwa wazi tena maduka makubwa yakiwa fwaaaaaaaa!

Kamati hiyo ikiwa na  uongozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa ilifika kufuatilia hali ya udhibiti wa uingizaji dawa, vyakula na vipodozi baada ya kuelezwa kuwa hali ni ngumu kutokana na mpaka ulivyokaa ambao hauna uzio hivyo kufanya shughuli za magendo kuingia kwa wazi bila kificho huku wengine wakiwa wamejenga nyumba zao kwa kuunganisha  mpaka.

Kufuatia hali hiyo wabunge hao walifika mpakani hapo na kupata maelezo kutoka kwa ofisa wa Uhamiaji eneo la Mpakani hapo bwana Evarist Mlay ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama mpakani hapo.

Ofisa huyo alitoa maeelezo juu ya hali ngumu ya udhibiti wa mpaka huo kutokana na nanmna ulivyo na akawaomba wambunge hao watembezwe kidogo ili awaonyeshe hali ilivyo ambapo eneo mojawapo ilionekana serikali ya zambia imelazimika kutengeneza barabara bubu ili kutambulisha mpaka huo baada ya watu wa Upande wa Tanzania kujenga hadi eneo la upande wa pili

kutokana na matembezi hayo yaliyochukua takribani kilometa mbili huku ofisa huyo wa Uhamiaji akionekana ama kwa makusudi anataka aonyeshe adha ambazo shughuli za wasimamizi wa sheria mpakani wanazipata, alianza kuwapitisha kando ya maduka yanayouza vipodozi vilivyopigwa marufuku vikiwemo Carolite, cream za kujichubua nk

Hali iliendelea kuwakatisha tamaa wabunge hao baada ya kufika eneo la Black Market ambapo shehena ya vipodozi imepangwa kwenye maduka ya jumla tena sehemu kubwa ni vile vilivyopigwa marufuku, ambapo wakalazimika kuuliza  kama kuna mahusiano yoyote baina ya pande hizo mbili katika utendaji wake

Katika kuonyesha kuwa suala la mipaka ni very complex kwa kimombo tena kwa msisitizo, walijibiwa kuwa upande wa Zambia hawana sheria  ya kuzuia bidhaa hizo hivyo wao wamewaachia watu wajiuzie, huku kwa upande wa Tanzania ambako ndiko soko kubwa linapatikana wakiwa wameweka sheria inayozuia vipodozi na dawa hizo.
Kwa upande wake ofisa wa  Idara ya Forodha ROGATIAN SHIRIMA akizungumza na kamati hiyo amesema achilia mbali matumizi ya teknolojia ya kutumia macho kukagua mizigo kwa kupekua mzigo manually! yaaani teknolojia ya Ujima! alisema hali hiyo inasababisha ukaguzi wa mizigo kuchukua muda mrefu na kuomba kurahisishiwa kwa kupata mitambo almaarufu kama scan equipment ambavyo vitakuwa vikikagua mizigo kidigitally badala ya analogia!!!

Aidha alizungumzia hali ya mpaka kuwa ni ngumu kudhibiti magendo kutokana na hali  ya uwazi na njia za panya nyingi na kwamba mapendekezo ya pamoja kwa idara zote zilizopo mpakani hapo ni kujenga ukuta kwa kila nchi ambao/ uzio utakaozunguka eneo lote la mpaka hivyo kuepeusha mazingira ya sasa ya kuwafanya wataalamu hao wanaelekea kuzidiwa kasi.

alisema kutokana na mianya hiyo magari yamekuwa yakipitisha bidhaa halamu na halali kwa kutumia njia za panya na kuingia upande wa pili wa mpaka ama kuingiza nchini pasipo vikwazo hali ambayo imechangia pia udhibiti mdogo wa bidhaa kama dawa, vyakula na vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku

wakichangia mjadala huo wabunge wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Profesa Maji Marefu walisema mazingira ya mpaka huo yanahitaji mjadala mpana kwa serikali ili kuona namna inavyoweza kusaidia kuondosha kasoro zilizopo.

mapicha yanakuja