Feb 16, 2013

KATIKA KUONYESHA KIU YA HUDUMA ZA AFYA,ANANCHI WAPOKEA KWA FURAHA ZAHANATI YA MSAMBA I

 WATOTO WALIKUWA WANAKATA MAUNO BALAAA KWENYE ILE KITU INAITWA UTAMADUNI
 BABU HUYU ALIKUWA BALAA KWA MIDADI WAKATI AKIKUNG'UTA NGOMA
 MAMA HUYU ANASEMA SASA BASI KWENDA KWA WAKUNGA WA JADI , DALILI ZINAZOONYESHA KUWA WANA MATUMAINI MAKUBWA NA HUDUMA ZA AFYA KIJIJINI MWAO
 HII NDIYO BENDI YA ZAKALE NI DHAHABU AMBAYO ILIKUWA IKITOA BURUDANI KWENYE MAADHIMISHO HAYO HUKU KIKOSI KIKIUNDWA NA WATU WENYE UMRI WA  KUSTAAFU UTUMISHI WA UMMA!

MZEE HUYU NAYE ALIKUWA MWANAKWAYA JANA 

 AKINA MAMA WAKITOA USHUHUDA WA MATUKIO YA VIFO NA CHANGAMOTO WALIZOPITIA KABLA YA KUKOSA HUDUMA ZA MATIBABU KIJIJINI KWAO
 MGANGA MKUU WILAYA YA MBOZI DR CHARLES MKOMBACHEPA AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI HUO, KUSHOTO KWAKE NI KATIBU WA AFYA WILAYANI MBOZI MZEE MROSSO NA KULIA KWAKE NI KATIBU TAWALA WILAYA BWANA LAZARO  MWANKENJA
JENGO LA ZAHANATI ILIYOZINDULIWA JANA KATIKA KIJIJI CHA MSAMBA I WILAYANI MBOZI

Na Danny Tweve -Mbozi


ASILIMIA 65  YA WANAWAKE WAJAWAZITO WILAYANI MBOZI MKOANI MBEYA BADO WANAJIHUJIFUNGULIA MAJUMBANI NA KWA WAKUNGA WA ASILI  HALI AMBAYO INASABABISHA  KUCHANGIA VIFO VINGI   VYA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA KUTOKANA  NA KUKOSEKANA KWA HUDUMA RAFIKI NA ZA KARIBU   ZA UZAZI SALAMA.

TAKWIMU ZA WILAYA ZINAONYESHA NI ASILIMIA 42 HADI 47 TU YA WANAWAKE WANAOJIFUNGULIA KATIKA VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI HUKU KUNDI KUBWA LIKIJISALIMISHA KWA WAKUNGA WA JADI NA WAGANGA WA KIENYEJI

HALI HII IMEELEZWA KUCHANGIWA NA UKOSEFU WA ELIMU NA HUDUMA HIZO KUWA MBALI NA WANANCHI 

HAYO YAMEBAINISHWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA MSAMBA I WILAYANI MBOZI AMBAPO WAMEREJEREA BAADHI YA MATUKIO YA HIVI KARIBUNI YA VIFO VYA WAJAWAZITO NA KWAMBA DHANA YA KILA KIJIJI KUWA NA ZAHANATI HAIPASWI KUPUUZWA KWA SASA KUTOKANA NA UKWELI KWAMBA CHANGAMOTO ZA MASUALA YA  UZAZI  NA MAGONJWA YA WATOTO  VIJIJINI NI NYINGI KUTOKANA NA KUKOSEKANA ELIMU YA AFYA YA MSINGI NA UZAZI SALAMA .

AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUFUNGUA ZAHANATI  ILIYOJENGWA KWA NGUVU ZA WANANCHI KIJIJINI HAPO MGANGA MKUU WA WILAYA YA MBOZI DR CHARLES MKOMBACHEPA AMESEMA, TAKWIMU ZA VIFO  VYA WATOTO NA WAJAWAZITO PAMOJA NA KIWANGO CHA HUDUMA ZA CHANJO ZINAONYESHA KUWEPO PENGO KUBWA LA HUDUMA KWA MAKUNDI HAYO ..

NAYE KATIBU TAWALA WA WILAYA MBOZI LAZARO MWANKENJA AMBAYE ALIMWAKILISHA MKUU WA WILAYA MBOZI KWENYE UFUNGUZI HUO AMEWATAKA WANANCHI KUJIELEKEZA KATIKA KUJENGA MIUNDO MBINU YA HUDUMA MBALIMBALI KWA NJIA YA KUJITOLEA ILI KURAHISISHIA SERIKALI KUELEKEZA RASLIMALI KATIKA UMALIZIAJI NA VITENDEA KAZI..

ZAHANATI HIYO KULINGANA  NA RISALA  ILIYOSOMWA NA BWANA JONATHAN MWAISWELO INALENGA KUTOA HUDUMA KWA WAKAZI  2,500 WA KIJIJI HICHO  HUKU PIA IKIWA NI FULSA MUHIMU KWA   VIJIJI JIRANI VYENYE WAKAZI ZAIDI YA 6500 

MUDA WOTE AKINA MAMA WALIKUWA WAKIIMBA NYIMBO NA KUFURAHIA HII IKIONYESHA KUCHOSHWA NA CHANGAMOTO ZA VIFO NA MAGONJWA MBALIMBALI KULIKOCHANGIWA NA KUKOSEKANA KWA HUDUMA ZA MATIBABU KWA KARIBU.

MWISHO