Mar 30, 2013

HUKUMU YA MAHAKAMA YA KENYA SOMO KWA MAHAKAMA ZINGINE AFRIKA MASHARIKI




JAJI  DR WILLY MUTUNGA WAKATI AKISOMA HUKUMU LEO
Uhuru Kenyatta rais mteule wa Kenya ataapishwa  April 09,2013 taarifa zinadokeza kutoka nchini humo.

Anachukua nafasi baada ya siku kadhaa  za mkwamo kufuatia kesi ya kupinga matokeo iliyowasilishwa na mpinzani wake Raila Odinga

Ushindi wa kesi kwenye makahama ya rufaa ya Kenya umeipa sura mpya Kenya katika safari ya kukua kwa demokrasia na uendeshaji wa mambo hii ikipongezwa na  watu mbalimbali wa kawaida na wale wenye viwango kipana vya tafakuri na fikra

Hii inatokana na ukweli kwamba jopo la majaji waliokuwa wakiongoza shauri hilo walivyoweza kusimamia msingi wa sheria wakati mawakili walipojaribu kuyumbisha mijadala ya kisomi na kisheria na kuipeleka kwenye mkondo wa siasa na utashi

Hukumu ya Dr Willy Mtunga iliyochukua dakika kumi kamili imeenda hatua kwa hatua katika kusoma hukumu yake kwa hoja nne zilizowasilishwa

Suala la kwanza lilikuwa kama uchaguzi uliendeshwa 3/march  katika hali ya haki na kidemokrasia na kwa kuzingatia katiba ya Kenya na sheria zake, mahakama imejiridhisha kuwa ulifanyika katika misingi hiyo

suala la pili lilihusiana na kura zilizoharibika kama kujumlishwa kwake ama kupunguzwa kwake hakukuwa na madhara ya kuathiri matokeo ya washindani, ambapo mahakama imeona kuwa kura zilizoharibika hazikuwa na mashiko ya kumbeba miongoni mwa wagombea kwa kuondolewa kwake ama kuongezwa
Dakika chache zijazo Raila Odinga atakuwa akitoa hotuba yake kwa wananchi wa kenya juu ya uamuzi wa mahakama kuu. endelea kufuatilia online kupitia KTN na NTV kupitia link ya blog ya indaba africa kulia
Hukumu ya kesi hiyo itakuwa tayari ndani ya wiki mbili ambapo wachambuzi na wasomi wataweza kuijadili kwa upana ingawa hawatakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi baada ya hapo kwakuwa mahaka hiyo ndiyo ya juu nchini humo ambapo hakuna uwezekano wa kufungua kesi ndani ya nchi hiyo kwa maamuzi ya mahakama ya rufaa.
Kwa ujumla mwenendo na uhuru wa mahakama ulionekana katika uendeshaji wa kesi hiyo ambapo vyombo vya habari vilikuwa huru kuripoti moja kwa moja mchakato mzima wa kutenda haki hadi hukumu ilipotolewa leo majira ya saa 11.30 jioni
Aidha hali ya kujiamini kwa majaji inatoa picha nyingine kuwa hapakuwa na msukumo wa utashi wa kundi fulani katika kuwafikisha katika maamuzi na badala yake walizingatia zaidi facts (hoja za kisheria) kulingana na vile zilivyowasilishwa na kama ziliathiri ama kuchangia utoaji maamuzi
Vyombo vya habari vya magharibi vimeendelea kusua sua kutoa maelezo hata breaking news za ushindi wa Kenyatta ambapo mitandao inaonyesha kucheleweshwa kwa habari hizo tofauti na wakati mwingine licha ya wandishi wa vyombo mbalimbali duniani kufatilia kwa karibu uchaguzi na maamuzi ya mahakama hiyo kuu
Chombo kimojawapo cbc news cha nchini Canada kimeandika mistari miwili juu ya hukumu hiyo na baadaye kuyumbia kwenye kesi inayomkabili kwenye mahakama ya kimataifa ambako huko maelezo yamekuwa mengi kushadihisha namna watakavyokabiliwa na mashitaka hayo

Mar 25, 2013

KIBAKA AUWAWA MBOZI JIONI HII, NI BAADA YA KUVAMIA KWA MUASIA

Huyu ndiye kibaka mzoefu kulingana na hukumu ya wananchi waliyoitekeleza katika eneo la Uhindini mjini Vwawa katika wilaya ya Mbozi ambako yeye akiwa na wenzake wawili wanatuhumiwa kuvamia na kupora kwenye nyumba ya mwananchi mwenye asili ya kiasia  na kuiba fedha na mali nyingine wakati mvua inanyesha mchana wa leo
 Marehemu ametambuliwa kwa jina la Joseph John Mapunda mkazi wa eneo la Ilolo katika mji wa Vwawa

 Picha zote na Mdau Chimika

Na Danny Tweve Mbozi
Mtu anayedhaniwa kuwa kibaka mkazi wa eneo la Ilolo Joseph John Mapunda ameuawawa na wananchi wenye jazba wakati akitekeleza uhalifu kwa kuvunja na kuiba katika moja ya nyumba zilizopangishwa na mtanzania mwenye asili ya asia katika eneo la sokoni mjini VWAWA wilayani Mbozi

Tukio hilo limetokea majira ya saa 9 alasiri  wakati mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika maeneo mengi ya wilaya ya Mbozi, kuonyesha kuathiri shughuli nyingi za mjini hapo kutokana na kuambatana na upepo mkali.
Fulsa hiyo ilikuwa mwafaka kwa vijana hao kufanya matukio ya uhalifu katika eneo la Nyumba ya jengo la SACCOS ya walimu mjini Vwawa na kujikuta mmoja akitumbukia kwenye mikono ya wananchi.

Kifo cha kijana huyo kimekuwa somo mbele ya jamii ambapo mkuu wa wilaya ya Mbozi akizungumza mara baada ya kuopolewa kwa mwili wake majira ya saa 12.40 kutoka kwenye kichaka kikubwa ambacho ni chanzo cha maji, kimezua gumzo kwa jinsi kijana huyo alivyofahamika kwa matukio ya hapa na pale toka enzi za utoto wake.


Mar 23, 2013

PRODUCTISHIZO!!!

 AAHHH BWANA TAKE TWOO!!!! UNAHARIBU SCEENE, YAANI UNAZUNGUMZA NA SIMU
 KAZI IMEANZA!
TAKE TWOO!!!!!

Mar 22, 2013

BIBI NA WAJUKUU

DIWANI WA VITI MAALUMU VWAWA AKIWASINDIKIZA WANAFUNZI WA SHULE YA MBOZI MISSION WAKATI WAKIREJEA KUTOKA SHULENI

MBOZI YAJIIMARISHA USIMAMIZI WA MIRADI

 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI LEVISON CHILEWA AKISISITIZA JAMBO WAKATI AKIKAGUA MIONGONI MWA MIRADI INATOTEKELEZWA WILAYANI MWAKE
 MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI ERICK MINGA AKIONYESHA KASORO KATIKA MOJA YA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA MKANDARASI AMBAPO ALIMTAKA MKANDARASI KUFANYA MAREKEBISHO
 DARAJA MUHIMU LINALOUNGANISHA ENEO LA HOSPITALI YA MBOZI MISSION AMBALO NI MIONGONI MWA MIRADI AMBAYO KUKAMILIKA KWAKE ITAWAKOMBOA WANANCHI KATIKA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI

WAKATI UKAGUZI UKIENDELEA, MWANANCHI HUYU HAKUWA NA HABARI KAMA KUNA WATU WANAFANYA KAZI AKAENDELEA NA SHUGHULI ZAKE KUNAWA MIGUU BURUDAAAAANI

Mar 21, 2013

A GOOD DAY

NAIKUMBUKA VIZURI SANA SIKU HII NIKIWA KWENYE REHERSAL YA MAHAFALI

SIKU MDAU AUGUSTINO NGETWA ALIPOACHA UKAPERA -RC KIHESA

WAZAMIAJI WA SHUGHULI WAKIWA KATIKA MAPOZI KAKANA DADA  NJE YA KANISA KATOLIKI LA KIHESA MJINI IRINGA

 SIJUI WAMEENDA WAPI? NDIVYO ANAVYOJIULIZA CHRISTIAN BAADA YA KUTELEKEZWA NJE YA KANISA WAKATI MAHARUSI WAKIWA WAMEINGIA KANISANI
 AKAPATA FULSA YA KUPIGA PICHA NA WASHIKAJI ALIOKUTANA NAO KWENYE MNUSO HUO
 MARA WAKAONGEZEKA WAKAWA WENGI CHRISTIAN NA DADA YAKE CHRISTABEL
 NGOJA NITOROKE
 OOOH DADA HUYOOOO!
 BWANA HARUSI AKIWA KWENYE POZI LA PICHA YA PAMOJA NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NJE YA KANISA KATOLIKI KIHESA
 PADRE ALIYREFUNGISHA NDOA AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MAHARUSI PAMOJA NA WAPAMBE WAO
KILICHOUNGANISHWA NA MUNGU MWANADAMU ASIKITENGANISHE

WAKATI MWINGINE TUJIPE MUDA WA MAPUMZIKO

AKINA MAMA HAWA WAKAZI WA MWENGE WILAYANI MBOZI WAKIWA KATIKA MAPUMZIKO BAADA YA KUPATA MLO WAO WA MCHANA ! NI MTU NA WIFI YAKE

KAZI KWELI KWELI, NAMWANDAA PAPARAZI WA KUENDESHA BLOG HII

MIAKA MICHACHE IJAYO  HUYU NDIYE ATAKAYEIONGOZA INDABA BLOG WAKATI MIMI NIKIWA NIMEISHIWA MBINU ZA UKAKAMAVU!!

MBOLEA FEKI INAWARUDISHA NYUMA WAKULIMA WETU

 MIFUKO YA MBOLEA FEKI ILIYOKAMATWA WILAYANI MBOZI IKIWA SOKONI KWAAJILI YA KUWABAMBIKIZIA WAKULIMA WAKATI WA MSIMU WA KILIMO! HALI HII IMEKUWA IKIREJESHA NYUMA JITIHADA ZA WAKULIMA

HAYA NDIYO MAMBO YA WATOTO WETU WA DIGITALI!!

HIVI NDIVYO WATOTO WETU WANAVYOKUA KWA KUJIFUNZA MAMBO YALIYONJE YA ULINGO WAO WA KUJIFUNZIA, BAADA YA KUZIDIWA MBINU AMEONA AWASILISHE YALIYO MOYONI KUPITIA UKUTA WA CHOO!!!
Add caption

MIRADI YA UMWAGILIAJI SASA KUMKOMBOA MKULIMA MBOZI




Huu ni mmoja wa miradi mikubwa ya umwagiliaji unaojengwa katika kijiji cha Iyula wilayani Mbozi, mradi wa skimu ya umwagiliaji unatarajiwa kuwanufaisha wakazi zaidi ya 600 katika eneo la umwagiliaji lenye hekta 300 katika tarafa ya Iyula

MAMA NA MWANA NDANI YA IRINGA

CHRISTIAN AKIWA NA MAMA YAKE KATIKA VIUNGA VYA MJI WA IRINGA HIVI KARIBUNI BAADA YA BABA YAO KUWAPA KITU INAITWA LOOK AND LEARN VISIT!

VIJANA WAWILI WAANZISHA KUNDI LA MZIKI WAKIWA NA UMRI WA MIAKA 8 NANE

KUNDI LA WASANII  CHIPUKIZI WA JIJINI MBEYA WANAOZUNGUKA NA KUZICHANGA KWA NJIA YA KUTOA BURUDANI KWA KUTUMIA GITAA LAO LA ASILI WAKIWA WANAFANYA MAMBO! JE UNASHAURI NINI KWA VIPAJI KAMA HIVI?

KWELI ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA!!

 PROFESA KATEGA MKUU WA KITIVO CHA SAYANSI YA MAZINGIRA NA DR MZIRAI MKUU WA IDARA YA UTAFITI, MACHAPISHO NA USHAURI  CHUO CHA MIPANGO DODOMA WAKIWA KATIKA MOJA YA MIJADALA CHUONI HAPO
TUKIO HILI BWANA LINA RAHA YAKE INAPOFIKIA HATUA YA KUPIGIWA TARUMBETA !!
 CLASS MET WANGU  ALMAARUFU WAJINA CHISOMI BIN MWALIMU WANGU AKIWA MFUATILIAJI KATIKA MOJA YA MIJADALA YA KITAALUMA  CHUONI HAPO

HUKU KWETU INAPOKUWA KWENYE MASUALA YA KIJAMII TUNA USHIRIKIANO 100%





KWAAJILI YA KUMBUKUMBU YA MDAU WETU NA RAFIKI YETU ALIYETUTOKA SIKU SI NYINGI

NYAMA BWANA!! WATU HAWAKUJALI KIBUDU

siku wananchi wa miji ya Tunduma, Vwawa na Mlowo walipolishwa vibudu baada ya wanachi kuvamia gari lililopata ajali likiwa limebeba ng'ombe kutoka Sumbawanga kupinduka eneo la OldVwawa darajani na kusababisha vifo vya ng'ombe zaidi ya 25, kwa mbaali katika picha wanaonekana wananchi wakiendelea kuchinja mizoga! huku mmoja akining'inia kwenye gari hilo

Mar 20, 2013

TAZAMA CHANNEL ZA RUNGINGA ZA KENYA HAPA


NA  
SASA UNAWEZA KUTAZAMA IDHAA ZA NTV  KENYA NA KTN LIVE KWA SAA 24  KUPITIA BLOG YA INDABA AFRICA