Mar 30, 2013

HUKUMU YA MAHAKAMA YA KENYA SOMO KWA MAHAKAMA ZINGINE AFRIKA MASHARIKI




JAJI  DR WILLY MUTUNGA WAKATI AKISOMA HUKUMU LEO
Uhuru Kenyatta rais mteule wa Kenya ataapishwa  April 09,2013 taarifa zinadokeza kutoka nchini humo.

Anachukua nafasi baada ya siku kadhaa  za mkwamo kufuatia kesi ya kupinga matokeo iliyowasilishwa na mpinzani wake Raila Odinga

Ushindi wa kesi kwenye makahama ya rufaa ya Kenya umeipa sura mpya Kenya katika safari ya kukua kwa demokrasia na uendeshaji wa mambo hii ikipongezwa na  watu mbalimbali wa kawaida na wale wenye viwango kipana vya tafakuri na fikra

Hii inatokana na ukweli kwamba jopo la majaji waliokuwa wakiongoza shauri hilo walivyoweza kusimamia msingi wa sheria wakati mawakili walipojaribu kuyumbisha mijadala ya kisomi na kisheria na kuipeleka kwenye mkondo wa siasa na utashi

Hukumu ya Dr Willy Mtunga iliyochukua dakika kumi kamili imeenda hatua kwa hatua katika kusoma hukumu yake kwa hoja nne zilizowasilishwa

Suala la kwanza lilikuwa kama uchaguzi uliendeshwa 3/march  katika hali ya haki na kidemokrasia na kwa kuzingatia katiba ya Kenya na sheria zake, mahakama imejiridhisha kuwa ulifanyika katika misingi hiyo

suala la pili lilihusiana na kura zilizoharibika kama kujumlishwa kwake ama kupunguzwa kwake hakukuwa na madhara ya kuathiri matokeo ya washindani, ambapo mahakama imeona kuwa kura zilizoharibika hazikuwa na mashiko ya kumbeba miongoni mwa wagombea kwa kuondolewa kwake ama kuongezwa
Dakika chache zijazo Raila Odinga atakuwa akitoa hotuba yake kwa wananchi wa kenya juu ya uamuzi wa mahakama kuu. endelea kufuatilia online kupitia KTN na NTV kupitia link ya blog ya indaba africa kulia
Hukumu ya kesi hiyo itakuwa tayari ndani ya wiki mbili ambapo wachambuzi na wasomi wataweza kuijadili kwa upana ingawa hawatakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi baada ya hapo kwakuwa mahaka hiyo ndiyo ya juu nchini humo ambapo hakuna uwezekano wa kufungua kesi ndani ya nchi hiyo kwa maamuzi ya mahakama ya rufaa.
Kwa ujumla mwenendo na uhuru wa mahakama ulionekana katika uendeshaji wa kesi hiyo ambapo vyombo vya habari vilikuwa huru kuripoti moja kwa moja mchakato mzima wa kutenda haki hadi hukumu ilipotolewa leo majira ya saa 11.30 jioni
Aidha hali ya kujiamini kwa majaji inatoa picha nyingine kuwa hapakuwa na msukumo wa utashi wa kundi fulani katika kuwafikisha katika maamuzi na badala yake walizingatia zaidi facts (hoja za kisheria) kulingana na vile zilivyowasilishwa na kama ziliathiri ama kuchangia utoaji maamuzi
Vyombo vya habari vya magharibi vimeendelea kusua sua kutoa maelezo hata breaking news za ushindi wa Kenyatta ambapo mitandao inaonyesha kucheleweshwa kwa habari hizo tofauti na wakati mwingine licha ya wandishi wa vyombo mbalimbali duniani kufatilia kwa karibu uchaguzi na maamuzi ya mahakama hiyo kuu
Chombo kimojawapo cbc news cha nchini Canada kimeandika mistari miwili juu ya hukumu hiyo na baadaye kuyumbia kwenye kesi inayomkabili kwenye mahakama ya kimataifa ambako huko maelezo yamekuwa mengi kushadihisha namna watakavyokabiliwa na mashitaka hayo