Apr 1, 2013

KIKUNDI CHA VIJANA WA KIKRISTO TUNDUMA CHASHINIKIZA NYAMA WALIYOCHINJA IUZWE



 HAPA NI BAADA YA KUFUNGULIWA KWA MABUCHA WANAYOYAITA YA WAKRISTO NA KUANZA KUUZA NYAMA KATIKA MJI WA TUNDUMA
 PAMOJA NA HALI HIYO YA MVUTANO  TUNDUMA SHUGHULI ZILIENDELEA KAMA KAWAIDA
 SHEIKH WA WILAYA YA MOMBA AKIZUNGUMZIA HATUA YA MAANDAMANO YA VIJANA WA KIKRISTO AMBAPO AMEOMBA WATULIE KWAKUWA JAMBO HILO LIPO KWENYE MAZUNGUMZO
 KIKUNDI CHA VIJANA WA KIKRISTO WAKIWA WAMEANDAMANA JANA MJINI TUNDUMA KUTAKA NYAMA WALIZOCHINJA ZIRUHUSIWE KUUZWA
 KIKUNDI CHA VIJANA WAKIWA WAMEBEBA BIBLIA NA MFANO WA MSALABA WAKIANDAMANA KUSHINIKIZA NYAMA WALIZOKUWA WAMEZICHINJA SIKU YA JUMAMOSI ZIRUHUSIWE KUUZWA MABUCHANI

 MOJA YA BUCHA ILIYOTANABAISHWA KWA IMANI KTIKA MJI WA TUNDUMA 

Kikundi cha Waumini wa kikristo katika mji wa Tunduma mkoani Mbeya jana mchana kimeongoza maandamano kupinga hatua ya mkuu  wa wilaya ya Momba Abiud Saidea kuzuia nyama iliyochinja na wakristo wenzao isiuzwe kwenye mabucha yao 

Hatua hiyo ni matokeo ya maelekezo ya mkuu huyo wa wilaya aliyoyatoa juzi kuwa nyama iliyochinjwa na wakristo kuzuiwa isigongwe mihuri na afisa afya wa eneo hilo tayari kwa kuuzwa na badala yake kuruhusu nyama iliyochinjwa na waislamu  igongwe mihuri na kuuzwa
Kutokana na hali hiyo watu waliochinja nyama hizo wakajikusanya  leo mchana baada ya kubaini kuwa walikuwa wakielekea kupata hasara kutokana na  tangazo hilo la serikali na hivyo kuamua kuandamana hatua ambayo ikalazimu mkuu wa wilaya kubadili maamuzi na kuwataka wakauze nje ya mji wa Tunduma.
Msimamo wa wauza bucha  ulikuwa nyama walizochinja waziuzie kwenye maduka yao ambayo wanafahamu wazi wateja wao ni wakristo. Hali hii ilizua ugumu wa kutoa maamuzi hadi maandamano yaliyoanza saa saba mchana kumsukuma afisa afya kugonga mihuri kwenye nyama zilizochinjwa na wakristu jana na kuanza kuuzwa.
Hadi kamera yetu inatoka eneo la Tunduma, tayari walikuwa wameshafikia mwafaka kuwa nyama iliyochinjwa na wakristo kwa mara ya kwanza jana mjini Tunduma iuzwe lakini baada ya hapo utaratibu huo usimame mpaka watapapofikia mwafaka katika majadiliano yanayoendelea baina ya viongozi wa kikristo na waislamu pamoja na kamati ya ulinzi na usalama  ya wilaya.
Sheikh mkuu wa wilaya ya Momba  anayeishi katika mji wa Tunduma Ahmed Omary anaeleza kuwa  vikao vya kufikia makubaliano ya suala la kuchinja baina ya waislamu na wakristu kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya bado vinaendelea hivyo ni vyema wananchi wakawaachia viongozi hao ili wafikie makubaliano
Kutokana na hali hiyo hali ya mji wa Tunduma kwa jumapili ya leo imekuwa katika hofu ingawa katika maandamano hayo hapakuambatana na vurugu zozote ambapo waongoza maandamano walitengeneza mfano wa msalaba na biblia vikitangulizwa mbele kwenye maandamano yao ingawa haijafahamika ililenga ujumbe gani.
Katika siku ya jana kwa sehemu kubwa ujumbe umetolewa makanisani kupitia waraka wa Tamko la muungano wa miamvuli ya makanisa nchini  TCF inayoshirikisha makanisa CCT, TEC, PCT na Waadventist kutaka serikali iache kuvunja katiba kwa kuingilia suala la uchinjaji na kuachia wakristo waendelee kujichinjia kwakuwa kuaachia waislamu kuchinja ni sehemu ya kutekeleza ibada ya  dini nyingine na hivyo kuingilia uhuru wa kikatiba wa kuabudu
Waraka huo mrefu uliosomwa na viongozi wa makanisa hayo, umegusia maeneo mbalimbali wanayoona serikali haijayatilia mkazo na kutaka ichukue hatua katika hoja zake walizoziorodhesha.