Mar 20, 2013

SHULE YA MSINGI MCHANGANYIKO YA MWENGE-MBOZI YAPATA BWENI LA WALEMAVU

 Bweni la watoto wenye ulemavu likiwa katika hatua za mwisho kukamilika, ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na halmashauri ya wilaya  ya Mbozi kwaajili ya kuweka miundombinu rafiki ya kusomea kwa watoto wenye ulemavu. Litagharimu kiasi cha shilingi 80 Milion mpaka kukamilika kwake
 Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mbozi Levison Chilewa  akijadiliana jambo na diwani wa Ihanda bwana Kasebele
 Badala ya kuwekwa ngazi, ngazi mchalazo kama hii ndiyo njia mwafaka ya kurahisisha walemavu kuingia kwenye jengo lao kuelekea darasani
 Vyoo vya walemavu vinavyoendelea kujengwa
Sura ya bweni kwa ndani na vibambaza vya vitanda