Mar 1, 2013

TETEMEKO LA ARDHI LATIKISA MBEYA

Na Danny Tweve wa indaba blog

Tetemeko la ardhi limetokea leo alfajiri majira ya saa 10.00 na maeneo mengi mkoani mbeya yameripotiwa kushuhudia hali hiyo

Wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi wamesema tetemeko hilo lilidumu kwa muda wa sekunde karibu 7 ambapo wengi walisikia mtikisiko na vyombo vya nyumani kuchezacheza.

Pia wakazi wa Tunduma wamekiri kusikia hali hiyo kama ambavyo pia wakazi wa Ipinda wilayani Kyela walivyothibitisha kutokea hali hiyo.

Aidha wakazi wa eneo la Lufilyo wilayani Rungwe wamethibitisha kutokea tetemeko hilo na pia kwa upande wa wilaya ya Ileje wakazi wa kijiji cha Igumbilo wamethibitisha kutikiswa na tukio hilo

Aidha kwa vijiji vya bonde la Kamsamba imethibitishwa kutokea pia hatua inayoonyesha kuwa bonde la lift valley kwa ujumla limeguswa na tetemeko hilo.

Kulikuwa na mshindo mkubwa wa muungulumo huku ikitokeza hali ya mtikisiko ambayo imechukua kati ya sekunde tano hadi saba saa 10 kamili usiku.' alieleza mmoja wa walioshuhudia tukio hilo.

hata hivyo blog hii haijaweza kufanya mawasiliano na watu wanaohusika na upimaji wa kiwango cha mtikisiko wa tetemeko hilo kutokana na ukweli kwamba hawa wataalam wapo mijini -Dar es salaam na hizi blog za vijijini kazi yake ni kuchokoza tu wenyewe watajitokeza kutoa facts!!!!