Katibu mkuu ofisi ya rais Ikulu Bw.Peter Ilomo(aliyekaa mwenye shati jeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya Mbozi baada ya kufanya ukaguzi wa miradi chini ya TASAF na ile ya MKURABITA
akionyeshwa ramani ya makazi ya eneo la karoleni mjini Tunduma ambako makazi yanatarajiwa kuhaulishwa ili kuruhusu ujenzi wa miundombinu kama barabara na mifumo ya maji taka huku wengine wakiwekewa utaratibu mzuri ikiwa ni pamojana kupatiwa hati
Miongoni mwa miradi chini ya Tasaf ambapo bweni la shule ya sekondari ya Isandula limekamilika na kufungwa umeme wa jua kuwawezesha watoto wa kike kusomea katika mazingira salama
Wanafunzi wakiimba wimbo wa Tanzania nakupenda kwa moyo wote! wakati katibu mkuu ofisi ya rais alipotembelea mradi wa bweni la shule yao
Mratibu wa TASAF MBOZI Bw. Hamis Mtoni mwenye tshirt ya njano akitoa ufafanuzi kwenye mradi wa ujenzi wa daraja linalounganisha eneo la Matengu na Old Vwawa lililojengwa na kaya zenye uhaba wa chakula kupitia TASAF awamu ya pili
Hapa akitembelea mradi wa mashine ya kukoboa mpunga ya watoto yatima katika mji wa Vwawa
akizungumza na watendaji katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi, kushoto kwake ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Levison Chilewa
Apr 30, 2013
Apr 25, 2013
MADIWANI WAUJIA JUU WARAKA KUTOKA TAMISEMI, KISA KUZIBA MIANYA
Na Indaba africa writter
Katika hali inayoonyesha TAMISEMI kugusa maeneo oevu ya baadhi ya mabaraza ya madiwani nchini, hatua yake ya kutoa waraka wa shughuli za ukaguzi wa miradi kufanywa na kamati ya Fedha,Utawala na Mipango FMU imeonekana kuwa mwiba mchungu kwenye baraza la halmashauri ya Mbozi leo baada ya waheshimiwa madiwani kutaka kuazimia kinyume cha kanuni maelekezo kutoka ngazi za juu! story kamili inafuata----
kutoka kushoto ni Makamu mwenyekiti ALAN MGULA, akifuatiwa na Mwenyekiti ERICK AMBAKISYE na akifuatiwa na DED MBOZI Levison Chilewa
michango ilianza hivi
Hawa watunga sheria wa baraza la Mbozi wakiwa hewani kama hivyo wakati kikao kikiendelea
Mh Emily Mzumbwe akichambua suala la uchangiaji wa hisa kwenye benki ya wananchi wa Mbozi ambapo limeonekana kurudisha reverse na madiwani baada ya kutaka mchakato huo usipelekwe puta kwa maelezo kuwa lazima wananchi waelimishwe pole pole namna ya kuchangia hisa zao badala ya kukata juu kwa juu sehemu ya fedha kwenye mauzo ya kahawa yao
Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya MBOZI wakisikiliza majadiliano
Kulia wa kwanza ni katibu tawala Mbozi bwana Lazaro Mwankenja akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mbozi bwana Levison Chilewa wakifuatilia upepo unavyokwenda kwenye baraza hilo
AFISA utumishi Bwana Zabron Lulandala akifuatiwa na afisa Mipango wilaya bwana Ngoi wakifuatilia mijadala kwenye baraza la madiwani leo
Baadhi ya watendaji kutoka ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya wakifuatilia mijadala kwenye baraza hilo leo
Hali hiyo ilijitokeza baada ya madiwani kupitia kamati zao kuanza kulalamika hatua iliyofikiwa ya kuzuiwa kwenda kukagua miradi wakiwa kwenye kamati zao na badala yake kupewa maelezo kuwa kuna waraka unaozuia kamati hizo kutokana na kukosekana ufanisi!
Ndipo miongozo mwenyekiti, azimio na maneno mengine ilipoanza kusikika, lakini mwishowe ikawa ngumu kurudisha wwaraka huo TAMISEMI na badala yake madiwani kukubaliana nao kwa shingo upande
Hatua hiyo ilifikiwa\ baada ya ufafanuzi kutolewa kuwa kimsingi serikali za mitaa pamoja na kuwa ni muhimili muhimu katika kuunganisha wananchi na kuleta maendeleo haimaanishi kuwa serikali kuu haina nguvu ya kuelekeza jambo mbele ya serikali za mitaa.
Na kwamba kwa kutambua hilo ndiyo sababu halmashauri kwa sehemu kubwa kama siyo asilimia 95% hutegemea ruzuku kutoka serikali kuu, hivyo pale inapoagizwa baadhi ya mabadiliko ngazi za chini hakuna lugha ya kuyapamba maelekezo hayo bali kuyatekeleza
Ndipo diwani mmoja akasimama na kuomba mwongozo kisha akachomekea na azimio! hata hivyo mwenyekiti wa baraza hilo akatoa ufafanuzi kuwa serikali haiwezi kuazimiwa kwakuwa baraza hilo limeundwa pia kutokana na maelekezo na miongozo kutoka juu hivyo waheshimiwa wawe wapole kwanza!
katika hatua nyingine suala la uanzishwaji wa benki ya wananchi ya Mbozi leo limeendelea kupigwa dana dana ya kukubaliana kuto kubaliana! baada ya madiwani kuunga mkono kuanzishwa kwa benki hilo lakini wakitaka wananchi waleweshwe pole pole na pia wapate ziara ya kwenda kujifunza mikoa mingine namna ya benki hizo zinavyofanya kazi
Katika hali inayoonyesha kuwa wimbi hilo lilishawekwa mapema, kila aliyenyanyuka alikuwa akiongezea misumali ya kuzuia kuharakishwa kuchangisha shilingi 200 kwa kilo ya kahawa kwaajili ya uanzishaji wa benki hiyo ambapo baada ya maelezo ya ufafanuzi ya mkurugenzi mtendaji wilaya ya MBOZI, bado suala hilo liliamuliwa kwa kutakiwa kwanza wapewe ziara na baadaye wananchi waelimishwe namna bora ya kushiriki uanzishaji wa benki hiyo.
indabaafrica blog

Apr 21, 2013
ISSUE YA UKIMWI-MADIWANI MBOZI WAPIGWA SHULE
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi wakisikiliza kwa makini wakti wakipata maelezo ya mchakato wa kuongeza hamasa ya kwa wananchi juu ya tohara, kwa ujumla mwitikio umekuwa mkubwa tangu operesheni ondoa mkono wa sweta iliyoanza mwezi huu kupitia hospitali ya wilaya ya Mbozi ambapo wastani wa watu 600 hujitokeza kila siku kunyofoa mikono ya sweta hata hivyo uwezo kwa siku ni watu 70tu!
Mh Makunganya akiwa anafuatilia mijadala
Mwenyekiti wa kamati ya Kudhibiti UKIMWI wilaya Mbozi CMAC mh Mgula akisoma kimemo "bila shaka kutoka kwa mmoja wa madiwani aliyetaka kujua vipande vya mikono ya sweta vinapelekwa wapi? kila anayefanyiwa suna angekuwa anapewa kipande chake akakifukie mwenyewe nyumbani!!!
Mwezeshaji na mnasihi katika hospitali ya wilaya ya Mbozi Bi Fumbo akifafanua jambo ambapo alieleza kuwa asilimia 80 ya wanawake wanabakwa licha ya kupata watoto kwenye kaya zao hawajawahi fika mshindo katika tendo la ndoa kutokana na akina baba kuwafakamia bila kuwaandaaa

Halmashauri ya wilaya ya MBOZI kupitia kitengo cha kudhibiti UKIMWI imeendesha warsha ya siku moja kwa wenyeviti wa kamati za kudhibiti UKIMWI za kata pamoja na mambo mengine kuzungumzia kampeni ya tohara kwa wanaume inayoendelea kutekelezwa kupitia hospitali ya wilaya ya Mbozi
Akizungumza kwenye warsha hiyo mratibu wa Kudhibiti UKIMWI wilaya Bwana Oscar Mgani alieleza kuwa katika kipindi kirefu wanachi wamekuwa wakihamasishwa kutoa mikono ya sweta, na sasa mwitikio umepanuka hadi kwa watoto wadogo
Katika hali ya kuonyesha watu wanakumbwa na aibu kwa kuendelea kuwa na mkono wa sweta baadhi ya wazee wenye umri mkubwa wamekuwa wakiongozana na watoto hadi hosipitalini wakidai wanawapeleka vijana wao kutahiri lakini wakishafika ndani kwenye eneo la upasuaji mdogo wao wenyewe ndiyo wanaanza kuvua suruali ili wapate huduma!
katika mijadala mbalimbali iliyoendeshwa katika warsha hiyo miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni umuhimu wa kuhamamasisha wananchi wanaoishi na vvu kujiunga na vikundi vya waVIU vijijini ili waweze kunufaika na fulsa zinazotolewa na serikali za mitaa pamoja na program za UKIMWI wilayani.
Apr 19, 2013
HAKI YA NANI VILE, WANANCHI MBOZI WALIZWA NA MBOLEA FEKI
Sehemu ya Mifuko ya Mbolea kimeo ikisogezwa pembeni na vijana wa kazi baada ya kufunguliwa kwa dula la Mbolea la STACO LTD na kusafishwa kwamba mbolea nyingine haina matatizo
Mbolea yenye alama ya kampuni ya YALA aina ya DAP ambayo pia imekutwa ikiwa chini ya kiwango
ofisa wa Upelelezi Mbozi akionyesha sehemu ya Mbolea mbovu ambayo imefumbiwa macho na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania na kuitakatisha kama haina matatizo wala madhara kwa wakulima
Katika hali inayoonyesha kuna mchezo mchafu wa kuendelea kuwamaliza wakulima wilayani Mbozi, shehena ya Mbolea mbovu iliyozuiwa kuuzwa mwaka jana hatimaye “upepo umepita” na kuruhusu iendelee kuuzwa kwamba ipo juu kiviwango!
Katika hali hiyo wakulima wamekuja juu jana wakati wakishuhudia ufunguzi wa duka la STACCO ambalo miezi kadhaa lilishuhudiwa likiwa limepigwa makufuli na kwa mbwembwe nyingi ikiwemo msururu wa vyombo vya habari, lakini kwa jana ilikuwa kimya kimya kufuli la kwanza likafunguliwa, likafuata la pili na hatimaye la tatu!
Wakati wananchi kwa macho yao meupe wakishuhudia mifuko iliyoganda ya Mbolea za UREA, DAP, CAN na SA taarifa iliyotolewa kuruhusu kufunguliwa kwa duka hilo inatoa maelezo kuwa ni Mbolea ya SA peke yake ndiyo iliyobainika kuwa na ubora hafifu! ambayo ni mifuko 11 tu.
Hata hivyo afisa anayesimamia ubora wa Mbolea katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi Bi Shonyela amesema licha ya maelekezo kutoka juu mengine hayatatekelezeka kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwamaliza wakuliwa wa wilaya yake kwakuzingatia kuwa Mbolea iliyoganda kuto kufaa tena mashambani.
“nimeandikiwa Mbolea aina ya SA pekee ndiyo isafirishwe chini ya usimamizi wa polisi kwenda Dar es Salaam lakini ni mifuko 11tu! Wakati kuna mbolea aina nyingine ambazo ni zaidi ya mifuko 50 hazina viwango vya ubora na taarifa imekuwa kimya” alifafanua
Uchunguzi wa haraka kwenye duka hilo unaonyesha kuwa mifuko16 ya DAP ilikuwa imeganda wakati wa kufunga duka hilo mwezi September mwaka jana, UREA mifuko 16, CAN 11 na SA 11.
Ingawa katika maelezo ya mkurugenzi wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA ilionyesha kuwa wangeshirikiana bega kwa bega na TBS katika kuhakikisha viwango vya bidhaa hiyo vinasimamiwa, maamuzi ya kuruhusu uuzwaji wa mbolea aina ya DAP, CAN na UREA iliyoharibika kwenye ghala la STACO wilayani Mbozi yanajenga mawimbi na mashaka kwa wananchi kuwa mamlaka imelainishwa na ama wamefumbishwa macho!
Tanzania hutegemea maabara yake ya Mbolea iliyopo Mlingano mkoani Tanga kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo hata hivyo kumekuwepo udanganyifu unaofanywa na baadhi ya maofisa wa serikali na kuwasaliti wakulima kutokana na makampuni yanayofanya shughuli za usambazaji wa pembejeo na hasa Mbolea kushika keki kubwa katika mzunguko wa fedha nchini
Wakati pia chuo cha kilimo SUA kimekuwa kikitumika katika tafiti na uchunguzi wa Mbolea, mwaka jana Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika Dr Adam Malima alikataa matokeo ya uchunguzi wa mbolea yaliyotolewa na SUA na kuahidi sampuli za Mbolea iliyokamatwa RUVUMA kupelekwa nchini Afrika kusini kujiridhisha na uchuguzi wa maabara za huko baada ya kulalamikiwa na wakulima
Aidha naibu waziri alisitisha leseni za makampuni ya STACO na Mohamed Enterpries mnamo August 07 mwaka jana, ambapo baada ya siku kadhaa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mbolea Tanzania Suzana Ikelya alitua Mbozi na kukamata Mbolea kwenye duka la STACO
“Maamuzi ya mamlaka ya ukaguzi wa ubora wa Mbolea yanawaacha wananchi wilayani Mbozi wakikosa imani kutokana na namna maamuzi yanavyofikiwa hata katika mambo ambayo hayahitaji utaalamu kuthibitisha ubora kama suala la Mbolea iliyoganda” anaeleza bwana Keneth Mwazembe mmoja wa wakulima wakubwa wilayani Mbozi.
Msimamizi wa duka la STACO bwana Julius Masai licha ya kufurahia kufunguliwa kwa ofisi yake ya chakula, amesema ni kweli kwamba kuna mbolea ambayo haimo kwenye barua ya kuruhusu uuzwaji ambayo haifai kwa matumizi lakini wanatumia busara kuitenga licha ya kutoelezwa kwenye barua hiyo
Ni kweli kuna mifuko kama 37 hivi ya mbolea mchanganyiko ambayo ni mbovu na tumeitenga pembeni na hatutaiuza” alisema meneja huyo bwana Julius Masai
Duka hilo limefunguliwa jana chini ya usimamizi wa maofisa wawili wa idara ya upelelezi ya jeshi la polisi na ofisa anayesimamia ubora wa MBOLEA wilaya ya Mbozi, na shughuli hiyo imefanyika kimya kimya tofauti na mbwembwe zilizofanyika wakati wa kufunga duka hilo ambapo wananchi waliokuwa wakipita barabarani waliitwa kushuhudia namna wanavyotendwa!
Apr 13, 2013
UWANJI CLASSIC HOTEL YAFUNGULIWA MJINI TUNDUMA, NI KIOTA KIPYA!!!!!
HOTEL MPYA YA UWANJI CLASSIC HOTEL YA MJINI TUNDUMA INAVYOONEKANA KWA MBELE
BANGO LA UPANDE WA HOTEL NA PUB AMBAPO WATU HUPATA RAHA ZAO KUANZIA CHAKULA BORA NA CHA KILA RADHA UNAYOITAKA NA KWA UPANDE WA PUB UTAPATA VINYWAJI VYA KILA AINA UNAVYOVITAKA
UNAPOFIKA UWANJI CLASSIC HOTEL, TAMBUA KUWA UMEKAMILISHA NDOTO YAKO YA USINGIZI WENYE SIFA ZOTE MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO HAPA DUNIANI.
KWA MALAZI YENYE VIWANGO VYA KIMATAIFA, NI UWANJI CLASSIC HOTEL
MENEJA WA HOTEL YA UWANJI AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WAKE KATIKA UTARATIBU WA KAWAIDA WA HOTEL MANAGEMENT KUPOKEA MAONI KUTOKA KWA WATENDAJI WA KILA SIKU
UKUMBI WA HOTEL, MAHALA PA KUPATIA CHAKULA UKIWA NADHIFU
UNAPOLALA UWANJI CLASSIC HOTEL USIWE NA HOFU NA HABARI YA KUOGA, WAKATI WOTE UNAPATA MAJI YA MOTO
HAPA NI PUB AMBAPO UTAKUNYWA KILE UNACHOTAKA, MADEREVA WA MAROLI YANAYOVUKA MIPAKA NJE YA TANZANIA WAMEKIRI KUWA HAPA NI MAHALA SAHIHI KWA WAGENI WANAOINGIA NA KUTOKA NJE YA TANZANIA
ULINZI NI WA UHAKIKA HUKU HOTEL IKILINDWA KWA MIFUMO YA KISASA ZIKIWEMO WAYA ZA UMEME ZILIZOZUNGUKA HOTEL HIYO
MKURUGENZI WA UWANJI CLASSIC HOTEL BWANA WILLY NGOGO AKIZUNGUMZA JANA NA INDABAAFRICA BLOG AMBAPO AMESEMA LENGO NI KUWAWEZESHA WAGENI KUFURAHIA MAISHA WAWAPO TUNDUMA NA MKOANI MBEYA KWA UJUMLA
WASILIANA NA UWANJI HOTEL KWA SIMU +255759559669,0655559669,0683559669
WAFANYAKAZI WA UWANJI HOTEL WAKIFUATILIA MAJADILIANO YALIYOONGOZWA NA MENEJA WA HOTEL HIYO LEO MCHANA
SEHEMU YA WAFANYAKAZI WAKISIKILIZA KWA MAKINI
BWANA NGOGO ANASEMA KUWA, MAANDALIZI YA UJENZI WA ONE STOP BORDER POST YANAYOENDELEA SASA KATIKA ENEO LA TUNDUMA NI MUHIMU YAENDE SAMBAMBA NA MIUNDOMBINU KAMA HOTEL NA HUDUMA ZINGINE ILI KUWAWEZESHA WATAALAMU WA UJENZI, VIONGOZI WA SERIKALI NA WADAU MBALIMBALI KUFURAHIA MAISHA YAO WANAPOKUWA KIKAZI KWENYE MIRADI HIYO NA KWAMBA UWANJI CLASSIC HOTEL NI SEHEMU YA MIKAKATI YA KUWEZESHA HUDUMA MUHIMU ZINAPATIKANA KATIKA MJI HUO